Zinazobamba

HALMASHAURI YA JIJI LA DAR INAYOONGOZWA NA UKAWA YAPEWA HATI SAFI,SOMA HAPO KUJUA

Pichani ni Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam,Isaya Mwita.
NA KAROLI VINSENT
MKAGUZI mkuu wa hesabu za serikali (CAG)Profesa Jumma Sad amepatia Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam hati safi baada kubainika kufanya matumizi sahihi kwenye fedha za umma.

Pia Mkaguzi huyo ameipongeza Hamashauri hiyo ambayo inaongozwa na vyama vya Upinzani kwa kuhakikisha wameongeza ukusanyaji wa mapato.

Akithibitisha kupewa hati hiyo safi mbele ya waandishi wa habari,Meya wa Jiji la Dar es Salaam,Isaya Mwita  amesema (CAG)  baada ya kuchunguza halmashauri hiyo amebaini Halmashauri hiyo kufanya matumizi mazuri ya fedha za umma katika mipango ya maendeleo.

‘Hii ni hatua nzuri kwetu CAG kaona matumizi mazuri sahihi ya fedha hakuna dosari ya ufisadi:’’Amesema Mwita.
Mwita ametaja sababu nyingine iliyopelekea kupewa hati safi ni Halmashauri kuongeza mapato kwenye vyanzo vyake vya awali.
“Tumeongeza mapato kwenye shirika la maendeleo la jiji  Dar es Salaam (DDC) Kutoka milioni 50 kwa mwaka hadi milioni 750 hii imepelekea mapato kuongezeka  na hata mkaguzi ametupongeza kwa hili“Ameongeza kusema Mwita.
Katika hatua nyingine Mwita amesema wanahakikisha kuendelea kutekeleza miradi mbali mbali ya maendeleo katika Halmashauri yake