Zinazobamba

PROFESA LIPUMBA AWATIMUA WABUNGE 8 WA CUF,SOMA HAPO KUJUA

Baraza kuu la chama cha wananchi CUF limewavua uanachama wabunge 8 wa viti maalum na madiwani wawili kwa kukiuka katiba ya chama hicho.

Akizungumza na wanahabari Dar es salaam muda mfupi uliopita mwenyekiti anayetambuliwa na ofisi ya msajili wa vyama vya siasa Prof Ibrahim Lipumba amesema wabunge hao na madiwani ambao waliitwa na kamati ya nidhamu ya chama hicho Jana kuhojiwa kutokana na kukiuka maadili ya uongozi hawakuweza kufika hata baada ya kupewa barua za kuitwa na kamati ya maadili hivyo baraza kuu limechukua maamuzi kwa kufuata katiba yake ya  mwaka 1984.

Lipumba amesema kuwa tuhuma zilizotolewa na kamati ya maadili ni pamoja na viongozi hao kupewa maelekezo na Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe  sambamba na kula njama ya kukihujumu chama hicho ikiwemo kushiriki operesheni iliyoandaliwa na Chadema iliyoitwa (Ondoa Msaliti Buguruni), jambo linalokiuka katiba ya CUF.

Wabunge na madiwani waliovuliwa uanachama ni pamoja na,
Riziki Shahali Ngwali, Saverina Mwijage ,Salma Mwassa ,Saumu Sakala,Riziki Lulida,Mgeni Jadi Kadika,Raisa Abdallah Mussa ,Miza Bakari ,Halima Ali Mohammed ,Khadija Al Kassim ,Leila Hussein Madibi Diwani Viti Maalum Ubungo pamoja na  Elizabeth Magwaja ambaye ni diwani Viti maalum Temeke.