MRITHI WA MAMA MGWIRA ACT-WAZALENDO HUYU HAPA,SOMA HAPO KUJUA
CHAMA Cha ACT-Wazalendo, kimemtangaza Yeremia Maganja kukaimu nafasi ya Mwenyekiti wa chama hicho, iliyokuwa imeachwa wazi na Anna Mghwira, aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, anaandika Shabani Matutu.
Msemaji wa ACT, Abdallah Khamis amesema Mwenyekiti Maganja, anatarajia kuanza kazi mara moja kwa kufanya ziara katika mikoa saba ya Tanzania bara ili kukagua uhai wa chama na maandalizi ya uchaguzi wa ndani ya chama ambao upo katika ngazi ya mitaa kwa sasa.
Ziara hiyo ya Mwenyekiti Maganja itaanza Julai 17 mwaka huu katika mkoa wa Mara pia atafuatana na Katibu wa Kamati ya Kampeni na Uchaguzi, Mohamed Massaga.
viongozi hao watakutana na kikao na kamati ya uongozi ya mkoa na majimbo yote ya mkoa Mikoa ya Simiyu (Julai 19), Shinyanga (Julai 20), Mwanza (Julai 21), Manyara (Julai 23), Arusha (Julai 24) na Kilimanjaro (Julai 25).
Baada ya ziara hiyo na itakayofuatiwa na tathmini ya kina Mwenyekiti Maganja atamalizia mikoa iliyosalia ya Tanzania Bara kabla ya kuelekea mikoani kwa ajili ya kujitambulisha rasmi.
Ziara hii ya Mwenyekiti Maganja itakuwa ni ya kwanza kwa kiongozi huyo ambaye alipokea kijiti cha uongozi kutoka kwa Mama Anna Mghwira, aliyeondolewa katika nafasi hiyo na kamati ya uongozi ya chama baada ya kuteuliwa na Rais John Magufuli kuwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro