TCRA YAPIGA FAINI KAMPUNI ZA SIMU,SOMA HAPO KUJUA
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imezitoza faini kampuni zote za simu kwa kusajili laini bila vitambulisho na kutofuata utaratibu.
Kampuni zilizotozwa faini hiyo na kiwango kikiwa kwenye mabano ni Airtel (Sh1.08 bilioni), Smart (Sh1.3 bilioni), Vodacom (Sh945 milioni), Zantel (Sh105 milioni) na Halotel (Sh1.6 bilioni).
Mkurugenzi wa TCRA, Mhandisi James Kilaba amesema leo (Julai 14) kuwa hii si mara ya kwanza kwa watoa huduma hao kukiuka sheria.
Kiliba amesema kutokana na kurudia kosa hilo, TCRA imeamua kuzitoza kampuni hizo faini hiyo.
Pia, kampuni hizo zimetozwa Sh500 milioni kila moja kwa kosa la kuathiri na kuhatarisha usalama wa umma na jamii ya Watanzania kwa kusajili laini bila kufuata utaratibu.