WAZIRI MKUU,KASSIM MAJALIWA AKIMWAGIA SIFA KIWANDA CHA NIDA,SOMA HAPO KUJUA
Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa leo ametembelea viwanda viwili vilivyochini yakampuni ya Namera Group of Industries inayomiliki viwanda vya Namera na NIDA, ambapo ameridhishwa na uwekezaji uliofanywa na uongozi wa kampuni hiyo.
Akizungumza Jijini Dar es Salaam Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema juhudi za Tanzania ya viwanda zimefanikiwa kwa asilimia kubwa kwani wawekezaji wengi na watanzania wanajitahidi kuanzisha viwanda hapa nchini huku akieleza kuwa kwa Mkoa wa Dar es Salaam kuna viwanda takribani 1845 ambavyo vimeajiri watanzania wengi.
[caption id="attachment_9117" align="alignnone" width="1024"]Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa ameambatana na Meneja Mkuu wa Kampuni ya Namera Group of Industries Muhammad Waseem.[/caption]
Waziri Majaliwa amevipongeza viwanda hivyo vya Namera na NIDA kwa kutoa ujuzi kwa wafanyakazi ambao waliingia kwenye ajira bila kuwa na ufahamu wa masuala mbalimbali ikiwemo kuzitumia mashine za kufumia mikeka na kutengenezea nguo.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Namara Group of Industries Muhammad Hamza (Mwenye suti ya mistari) na Meneja Mkuu wa kampuni hiyo Muhammad Waseem (Mwenye suti ya bluu).[/caption]
Katika hatua nyingine Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliweza kuzungumza na wafanyakazi wa kiwanda cha NIDA kilichopo maeneo Tabata, ambapo amewasihi wafanyakazi hao kuitumia fursa hiyo vizuri ya kufanyakazi katika kiwanda hicho cha NIDA kwa kuwa waadilifu na waaminifu ili wawe mabalozi wema na Tanzania ipate sifa ya kuwa na wafanyakazi wenye uadilfu jambo ambalo litawavutia wawekezaji wengine.
Kwa upande wa wawakilishi wa wafanyakazi hao Ahmed Kiumbe alimuomba Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kushughulikia suala la nyongeza ya mshahara kima cha chini 150,000 ili waweze kumudu gharama za maisha kwani kiwango wanacholipwa na kampuni hiyo kwasasa hakitoshi kiwango cha 800,00 mpaka 100,000 jambo linalopelekea wao kuishi maisha magumu.
"Mwaka jana alikuja Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde na alituhaidi kulishughulikia suala la nyiongeza ya mshahara alipotembelea kiwanda hiki lakini mpaka sasa tunaona kimya na kiwango ni kilekile" Alisema Kiumbe muwakilishi wa wafanyakazi NIDA.
Akijibu suala hilo Waziri Mkuu Majaliwa ameeleza kuwa atamuagiza Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde ili siku ya Jumatatu aje kuzungumza na wafanyakazi hao na kuangalia namna gani wanaweza kulitatua suala hilo lenye maslahi ya wafanyakazi.
Pia amemtaka Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo Muhammad Hamza kushughulikia changamoto hiyo na kuendelea na upanuzi wa kiwanda hicho kwa faidia yao na watanzania kwa ujumla.
[caption id="attachment_9097" align="alignnone" width="1024"]Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema (Kulia) akiambatana na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Namara Group of Industries Muhammad Hamza.[/caption]
Ziara hiyo ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Theresia Mbando, Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema, Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo, Naibu Mstahiki Meya Wilaya ya Ilala Omary Kumbilamoto na viongozi mbalimbali.
Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa leo ametembelea viwanda viwili vilivyochini yakampuni ya Namera Group of Industries inayomiliki viwanda vya Namera na NIDA, ambapo ameridhishwa na uwekezaji uliofanywa na uongozi wa kampuni hiyo.
Akizungumza Jijini Dar es Salaam Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema juhudi za Tanzania ya viwanda zimefanikiwa kwa asilimia kubwa kwani wawekezaji wengi na watanzania wanajitahidi kuanzisha viwanda hapa nchini huku akieleza kuwa kwa Mkoa wa Dar es Salaam kuna viwanda takribani 1845 ambavyo vimeajiri watanzania wengi.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa ameambatana na Meneja Mkuu wa Kampuni ya Namera Group of Industries Muhammad Waseem.
Waziri Majaliwa amevipongeza viwanda hivyo vya Namera na NIDA kwa kutoa ujuzi kwa wafanyakazi ambao waliingia kwenye ajira bila kuwa na ufahamu wa masuala mbalimbali ikiwemo kuzitumia mashine za kufumia mikeka na kutengenezea nguo.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Namara Group of Industries Muhammad Hamza (Mwenye suti ya mistari) na Meneja Mkuu wa kampuni hiyo Muhammad Waseem (Mwenye suti ya bluu).
Katika hatua nyingine Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliweza kuzungumza na wafanyakazi wa kiwanda cha NIDA kilichopo maeneo Tabata, ambapo amewasihi wafanyakazi hao kuitumia fursa hiyo vizuri ya kufanyakazi katika kiwanda hicho cha NIDA kwa kuwa waadilifu na waaminifu ili wawe mabalozi wema na Tanzania ipate sifa ya kuwa na wafanyakazi wenye uadilfu jambo ambalo litawavutia wawekezaji wengine.
Kwa upande wa wawakilishi wa wafanyakazi hao Ahmed Kiumbe alimuomba Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kushughulikia suala la nyongeza ya mshahara kima cha chini 150,000 ili waweze kumudu gharama za maisha kwani kiwango wanacholipwa na kampuni hiyo kwasasa hakitoshi kiwango cha 800,00 mpaka 100,000 jambo linalopelekea wao kuishi maisha magumu.
"Mwaka jana alikuja Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde na alituhaidi kulishughulikia suala la nyiongeza ya mshahara alipotembelea kiwanda hiki lakini mpaka sasa tunaona kimya na kiwango ni kilekile" Alisema Kiumbe muwakilishi wa wafanyakazi NIDA.
Akijibu suala hilo Waziri Mkuu Majaliwa ameeleza kuwa atamuagiza Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde ili siku ya Jumatatu aje kuzungumza na wafanyakazi hao na kuangalia namna gani wanaweza kulitatua suala hilo lenye maslahi ya wafanyakazi.
Pia amemtaka Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo Muhammad Hamza kushughulikia changamoto hiyo na kuendelea na upanuzi wa kiwanda hicho kwa faidia yao na watanzania kwa ujumla.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema (Kulia) akiambatana na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Namara Group of Industries Muhammad Hamza.