JIJI LA DAR CHINI YA UONGOZI WA CHADEMA LAPATA HATI SAFI KUTOKA KWA CAG
Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita akizungumza na wajumbe wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya jiji, aliyekaa kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa jiji Waziri Kombo. |
HALMASHAURI
ya jiji la Dar es Salaam imepata hati safi kupitia taarifa ya Mkaguzi
na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha
2015/2016.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini hapa mara baada ya kumalizika kwa baraza
la madiwani la halmashauri ya jiji iliyokuwa na ajenda moja ya
kuwasilisha taarifa ya CAG, Mstahiki Meya Isaya Mwita alisema kuwa hati
hiyo imetokana na kuwepo kwa usimamizi mzuri wa matumuzi ya fedha.
Alifafanua
kuwa kwa kiasi kikubwa tangu alipochaguliwa kushika nafasi hiyo ,jiji
la Dar es Salaam lilisimamia na kupunguza matumizi ya fedha ambayo
hayakuwa ya lazima jambo ambalo limeleta heshima kubwa katika
halmashauri hiyo.
Aliongeza
kuwa mbali na hiyo, lakini pia kwa kiasi kikubwa mapato ya jiji
yameongezeka kutokana na kusimamia kikamilifu vyanzo vya mapato
vilivyopo ndani ya jiji hilo.
Alifafanua
kuwa hati hiyo inaleta heshma kubwa ndani ya jiji na kwamba imetoa
nafasi kwa watendaji ndani ya halmashauri kufanya kazi kwa umahiri zaidi
ili kuweza kuleta maendeleo makubwa kwa wananchi.
Alisema
taarifa ya CAG imeeleza wazi kuwa hali ya utekelezaji ndani ya jiji ni
ya kuridhisha kutokana na usimamizi wa kutosha ,kufuatilia mambo na
hivyo kuweza kuyafanyia kazi mapendekezo ya ukaguzi wa miaka ya nyuma
yaliyosalia.
“ Baada
ya kupata hati hii, sasa niwakati mwingine jiji kuendelea kufanya kazi
za kuwatumikia wananchi ili waweze kunufaika na rasilimali zao,
ukiangalia tumepewa dhamana kubwa ya kuwatumikia ,hivyo kama Meya mwenye
jiji sina budi kuwatumikia wananchi kama inavyotakiwa” alisema Meya
Mwita.
Aidha
Meya Mwita alitoa wito kwa halmashauri zilizopo ndani ya jiji la Dar es
Salaam kuwatumikia wananchi ikiwemo kutatua kero zinazo wakabili.
Wakati
huo huo ,Meya Mwita alisema kuwa jiji limetenga shilingi milioni 500
kwa ajili ya kununua maeneo ya makaburi kutokana na kuwepo kwa
changamoto ya maeneo ya kuzikia watu.
Alisema
kwasasa hali imekuwa mbaya kwenye maeneo ya jiji na kwamba pesa hizo
zitatumika kununua maeneo ambayo yatatumika kwa ajili ya kuzikia watu
wanapopoteza maisha.
“
Jambo hili litaanza kufanyika mwaka huu, kila halmashauri itapatiwa
eneo kwa ajili ya kuzikia watu, yapo maeneo ambayo tumepanga kuyanunua,
ukiangalia jiji letu lina watu wengi sana, kadiri siku zinavyozidi
kwenda ndivyo watu wanavyozidi kuongezeka