SHEREHE ZA UWEKAJI WA JIWE LA MSINGI LA MRADI WA MAFUTA GHAFI TOKA HOIMA NCHINI UGANDA HADI TANGA KUFANYIKA AGOSTI 5, 2017
10:06:00 AM
Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani anawaalika
wananchi katika halfa ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa bomba la
mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanga, Tanzania.
Uzinduzi huo unatarajiwa kufanyika Agosti 5, 2017 eneo la Chongoleani
jijini Tanga ambapo utahudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Rais wa Jamhuri ya Uganda
Mhe. Yoweri Museveni.
UDUGU WETU, FAHARI YETU - BOMBA LETU KWA MAENDELEO YA WATU WETU