Zinazobamba

WALEMAVU WALIA KUDHALILISHWA...WAZIRI MWENYE DHAMANA AOMBA RADHI

 
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu Kikishirikiana na Taasisi ya za Binadamu na Maendeleo ya Kiuchumi kwa Watu Wenye Ulemavu wamelaani vikali kitendo kilichofanywa na Jeshi la Polisi cha kuwapiga na kuwadhalilisha walemavu wakati wakiwa kwenye madai yao ya msingi. 
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu Bi. Anna henga(kulia) na pembeni yake ni Mkurugenzi Mtendaji Taasisi ya Haki za Binadamu na Maendeleo ya Kiuchumi kwa watu wenye Ulemavu Bw. David Nyendo wakiongea na waandishi wa Habari mapema leo jijini Dar es salaam

Akiongea na Waandishi wa Habari Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Bw. David Nyendo alisema kuwa wanasikitishwa na Polisi kwa kuweza kutumia nguvu kubwa ya kana kwamba wanapambana na majambazi kumbe ni watu wenye ulemavu. Kujichukulia Sharia mkononi pia ni kosa kwani chombo pekee chenye mamlaka ya kutoa hukumu ni Mahakama. “Kitendo cha kuwapiga, kuwaburuza na kuwadharirisha Walemavu ni kinyume cha Sharia na kinafaa kupingwa na kila Mwananchi”.alisema

Hivyo kufuatia yote hayo Jeshi la Polisi limetakiwa kutekeleza mambo kadhaa ikiwa ni fidia kwa watu wenye ulemavu kwa kuwadhalilisha na kuwaumiza.

Jeshi la Polisi kuacha kutumia nguvu kubwa iliyopitiliza ili kuweza kulinda haki za walemavu na Raia wa kawaida kwani kufanya hivyo ni kuvunja misingi ya utoaji haki.

Ndani ya siku saba Jeshi la Polisi Kanda ya Dar es salaam na Mkuu wa Jeshi la Polisi kuomba msamaha kwa njia yeyote ile itakayoona ni vema, ikiwa ni kujitkeza  hadharani kuwaomba msamaha watu wenye Ulemavu na Taifa kwa ujumla kwa kitendo cha udhalilishaji kilichofanywa na maafisa wake mnamo tarehe 16/6/mwaka huu. Kwani kinyume na hapo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya jeshi hilo.

Sanjari na hayo yote Jeshi la Polisi limetakiwa kutoa fidia ama nafuu kwa waathirika wa shambulizi hilo.

    Kutoa Baiskeli za Walemavu 30 ambazo ziliharibiwa kutokana na shambulio hilo.
Kulipa fidia kwa wale wote waliolipotiwa kupotelewa na mali zao kama fedha na simu kwenye shambulio hilo.
 
 
 WAZIRI AOMBA RADHI WALEMAVU

 Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba leo ameomba radhi bungeni mjini Dodoma kwa kitendo kilichofanywa na askari polisi cha kuwadhibiti kwa kutumia nguvu kubwa watu wenye ulemavu Jijini Dar es salaam. Amesema kuwa jeshi la polisi lilitumia nguvu kubwa mno kuwadhibiti watu hao na kusema kuwa wao kama Serikali wamelipokea jambo hilo na ameahidi kulifanyia kazi ili lisiweze kujirudia tena.
“Kwanza naomba niombe radhi kwa jambo hili na naomba salamu zangu ziwafikie watu wenye ulemavu, ni kweli kwamba kwa kuzingatia hali yao jeshi la polisi lilitumia nguvu kubwa, ila sisi kama serikali tumeshawasiliana na TAMISEMI na kuzungumza nao juu ya mambo yao, lakini pia tumepokea jambo hili na tunalifanyia kazi ili siku nyingine jambo hili lisijirudie,” amesema Nchemba.
Hata hivyo, watu hao wenye ulemavu mnamo tare 16 June 2017 walishambuliwa na jeshi la polisi Jijini Dar es salaam kwa lengo la kuwatawanya walipokuwa wamekusanyika kwaajili ya kutaka kwenda kumuona Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala kuwasilisha malalamiko yao ya kuzuiliwa kuingia katikati ya jiji ili waweze kufanya shughuli zao.