WALEMAVU SASA WAOMBA KUPEWA VITUO VYA KUPAKIA NA KUSHUSHA ABIRIA KATIKATI YA JIJI
Mwenyekiti
wa Chama cha watu wenye ulemavu kwa Mkoa wa Dar es Salaam Ahmad
Abdallah Komboza ameiomba serikali ya Mkoa wa Dar es Salaam kupitia
Mkurugenzi wa Halmashauri ya jiji kuwatengea vituo vya kushushia na
kupakia abiria ili kuondoa sintofahamu baina yao na jeshi la polisi
Mwenyekiti
huyo ameeleza kuwa jeshi la polisi limekuwa likiwakamata kwa kosa la
kutokuwa na vituo maalum vya abiria na kuwatoza kiasi kikubwa cha fedha
mpaka kufikia elfu 90 jambo ambalo linawarudisha nyuma kimaendeleo.
Pia
amelaani kitendo kilichotokea Juni 16 kwa jeshi la polisi kuzuia
maandamano yao ya amani kwa madai ya kutokuwa halali kisheria na kudaiwa
kuwapiga na kuwajeruhi baadhi ya walemavu wapatao 40 na kuwapeleka
katika vituo vya polisi huku bajaji 76 zikikamatwa, hivyo ameomba
walipwe fidia na jeshi la polisi liombe radhi kwa tukio hilo na iwe
mwisho wa matukio hayo.
Huku
akisisitiza kuwa walipanga kwenda kwa Mkurugenzi kusisitiza madai yao
ya vituo vya abiria, ndipo polisi wakaja na kuzuia maandamano hayo.
Kwa
upande wake Charles Temba Katibu wa Umoja wa Waendesha Bajiji Mkoa wa
Dar es Salaam ameeleza kuwa suala la vituo vya abiria wametuma maombi
kwa serikali tangu mwaka 20tano na waliainisha baadhi ya maeneo 20
ambayo walipendekeza yawe rasmi kwa waendesha bajaji walemavu ikiwemo
Feri, Mnazi Mmoja, Upanga, Shule ya Uhuru lakini mpaka sasa hakuna
kilichoshughulikiwa.
"Tulitoa
mpaka nakala na kuziwasilisha ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya,
Meya wa Jiji na Mkurugenzi ambapo tuliainisha mapendekezo ya vituo 20
vya abiria lakini mpaka sasa ombi letu halijashughulikiwa na tunazidi
kutozwa kwa kosa la kutokuwa na vituo maalum vya kupaki abiria"
Katika
hatua nyingine Mwendesha bajaji Fatuma Amrani Abdallah amelomba jeshi
la polisi kutotumia nguvu kwa watu wenye ulemavu kwani wao ni kundi
maalum linalohitaji kuangaliwa kwa upekee, vitendo vya kuwapiga na
kuwatolea lugha chafu havifai , hivyo mamlaka husika inabidi ichukue
hatua stahiki, kwani Tanzania ni nchi inayosifika kwa amani.