Zinazobamba

KIGWANGALAA AFUNGUKA,ASEMA HAYA KUHUSU SAKATA LA MADINI,SOMA HAPO KUJUA

Kupitia ukurasa wa kijamii wa twitter wa Mbunge wa Nzega Vijijini, Dk. Hamisi Kigwangalla ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, ameweka wazi kuwa daima ataendelea kupambana dhidi ya rasilimali za umma, kwani amekuwa mwanaharakati kwa muda mrefu.

“Tuliopinga wizi wa madini yetu tulibezwa, tulikamatwa kama wezi; tuliswekwa ndani, tulionekana wasaliti. Leo kiko wapi? #NasimamaNaRaisWangu” aliandika Dk. Kigwangalla huku watu mbalimbali wakitoa maoni yao.

Kwa mujibu wa Dk. Kigwangalla amebainisha kuwa, suala la kupambana na rasilimali za Taifa alilianza miaka mingi kwani miongoni mwa matukio makubwa ni la 2013, ambapo alijitolea kupambana kudai haki  tukio lililopelekea kutiwa nguvuni na Jeshi la Polisi.

Dk. Kigwangalla anasema  katika kupigania maslai Taifa ataendelea kuunga mkono juhudi za Rais Dk. Magufuli  mwanzo mwisho kwani ni moja ya matunda ya nchi yoyote ile Duniani.

Anasema kiongozi Mkuu lazima alinde na kupigania rasilimali za nchi, hivyo akiwa Mtanzania na kiongozi mwenye dhamana anaunga juhudi hizo bila kuchola.

Tuliopinga wizi wa madini yetu tulibezwa, tulikamatwa kama wezi; tuliswekwa ndani, tulionekana wasaliti. Leo kiko wapi? 

A