RAIS MAGUFULI AMTUMBUA KIAINA BOSI WA DAWASA JUKWAANI,SOMA HAPO KUJUA
Rais John Magufuli amemtaka Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (Dawasa) Archado Mtalemwa ajiandae kustaafu kutokana na mapungufu mengi ambayo Rais amesema ameyaona katika mamlaka hiyo.
Rais ameyasema hayo leo(Jumatano) akiwa katika ziara yake ya siku tatu mkoani Pwani na alitumia fursa hiyo kuzungumzia miradi ya maji na ulipaji wa maji kwa taasisi za serikali.
“Ndugu yangu Mtalemwa, naongea kwa lugha nzuri hapa, nikuombe tu kuwa ustaafu mapema, inawezekana Waziri wa Maji ni rafiki yako, kama ilivyo kwa mawaziri wengine, lakini nadhani huu ni wakati mzuri,”amesema na kuongeza;
“Pamoja na kazi zako nzuri, it’s your time to go.”
Rais Magufuli amezungumzia kero mbalimbali za maji na kusema kuna upotevu mkubwa wa maji.