Zinazobamba

VURUGU NDANI YA CUF,PROFESA LIPUMBA AYATUMA ''MAZOMBI' KUVAMIA MKUTANO WA MAALIM SEIF,SOMA HAPO KUJUA

Dar es Salaam. Watu wasiofahamika wamevamia mkutano wa wanachama wa CUF upande unaomuunga mkono, Katibu Mkuu wa Chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad.

 Mkutano huo uliokuwa ukifanyika katika Hoteli ya Vina, Mabibo, ulipangwa kuanza leo saa tano asubuhi lakini kabla haujaanza watu waliovalia soksi nyeusi usoni(mask) walivamia na kuanza kuwapiga wanachama wa CUF na waandishi waliokuwa kwenye mkutano huo.

Akizungumza na Muungwana blog Mwenyekiti wa chama hicho wa wilaya ya Kinondoni Juma Mkumbi amethibitisha kuvamiwa na watu aliyedai kuwa ni wafuasi wa Profesa Lipumba.

Mkumbi ameeleza kuwa watu hao walifika eneo hilo wakiwa na gari aina ya cruiser mbili zenye bendera ya chama cha CUF.

Ameeleza kuwa manusura yao yalipatikana baada ya wananchi wa eneo hilo kuwaokoa kutoka kwa wavamizi hao.

Polisi imeshafika eneo la tukio na inawahoji wanachama hao wanaomuunga mkono Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad waliokuwa wakifanya mkutano wao wa ndani.

 Pia Polisi inawahoji waandishi wa habari waliopo eneo la tukio.