DKT BILAL AWATAKA WANANCHI NA TAASISI MBALI MBALI KUJITOSA KWENYE VITA DHIDI ZA UKIMWI,SOMA HAPOKUJUA
MAKAMU wa
Rais mstaafu,Dkt Muhamed Galib Bilali amesema suala la kuchangisha fedha za
kusaidia kutomeza na kuzuia maambukizo dhidi ya virusi vya Ukimwi sio jukumu la
serikali pekee yake bali ya jamii nzima.
Dkt Bilali
ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam
wakati wa Halfa ya kuchangisha fedha kwaajili
ya kusaidia vita ya kupambana na maambukizi ya virusi vya Ukimwi ambapo katika
Halfa hiyo iliyoandaliwa kwa pamoja na Mgodi wa Geita Gold Mine (GGM) kwa
kushirikiana na Tume ya
Dkt Bilal
amesema jamii inahaja ya kuungana na
kujitoa kwa kuhakikisha jamii inaondoana na maambuki ya ugonjwa wa Ukimwi.
‘’Ungonjwa wa
Ukimwi umekuwa ukichangia kuzorotesha nguvu ya wananchi katika kujiletea maendeeo,hivyo licha ya
jitihada za serikali katika kuhakikisha
wanakomesha ugonjwa huu ,pia wananchi kwa ujumla wanatakiwa kuungana na
serikali katika kuhakikisha wanachangia katika kutoa mchango wao kuhakikisha
tunakomeza ugonjwa huu’’Amesema Dkt Bilal.
Kwa Upande
wake Mkurugenzi wa (TACAIDS) Dkt Leonard Mabelo amesema licha ya takwimu kuonyesha
maambukizi ya virusi vya ukimwi
yamepungua, pia jamii inahitajika kujitoa na kuhakikisha ungonjwa huo
unaondokana katika jamii kwa kujitoa mchango wao kwa hali mali kwenye taasisi za
kupambana na virusi vya Ukimwi kuhakikisha ugonjwa huo unaondokana kwenye
jamii.
Pamoja na hao,naye
Mkurugenzi wa (GGM)Richard Jordinson amesema Kampuni hiyo itaendelea kutoa mchango wao wa hali na
mali katika kufanikisha mapambano hayo yanafanikiwa.