Zinazobamba

DKT BILAL MGENI RASMI UZINDUZI WA KAMPENI YA KILL CHALLENGE 2017,SOMA HAPO KUJUA



Pichani ni Makamu wa Rais  wa mradi endelevu wa Mgodi (GGM) ,Simoni Shayo akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu uzinduzi wa Kampeni ya Killchallenge 2017 

MAKAMU wa Rais mstaafu wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania  wa  serikali  ya awamu nne,Dkt Muhamed  Ghalib Bilal anatarajia kuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa  kampeni ya Kill Challenge kwa mwaka 2017 ,kampeni hiyo yenye  lengo la kukusanya fedha kwa ajili kusaidia mapambano dhidi ya maambukizi ya vurusi vya Ukimwi.
Kampeni hiyo ambayo imeandaliwa na   Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) kwa kushirikiana na Tume ya kupambana na virusi vya Ukimwi  nchini (TACAIDS).
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam, Makamu wa Rais  wa mradi endelevu wa Mgodi (GGM) ,Simon Shayo  amesema uzinduzii huo utafanyika leo  Jioni kwenye Hotel ya kimataifa  Kilimanjaro  Hoteli .

‘’Nawakalibisha watu wote kujitokeza katika kuchangia fedha hizi ili zisaidie katika kupambana na maamumbuki haya,kwani jukumu la kupambana na ugonjwa huu sio wa serikali peke yake bali hata jamii nzima inahaja ya kujitokeza na kupambana na ugonjwa huu’’Amesema Shayo.

Shayo amebainisha kuwa  katika kampeni hiyo wameshirikiana na wasanii akiwemo Mrisho  Mpoto kwa lengo la kuiamsha jamii ili ijitokeze katika kupambana na vita hiyo.


Oichani Mkurugenzi wa Tume ya kupambana na virusi vya Ukimwi  nchini (TACAIDS).Dkt Leonard Maboko akizungumzia Kampeni hiyo


Kwa upande wake mkurugenzi wa (TACAIDS)Dkt Leonard Maboko amewasihi Makampuni mengine yaige mfano  wa (GGM) Katika kuhakisha watahakikisha ugonjwa wa Ukimwi unatokomezwa nchini.






Pichani  ni Msanii Mrisho Mpoto ambaye ni Blozi wa  Kampeni hiyo pia amewasanii wasanii wenzake kujitokeza katika mapambano ya ukimwi