MWENDO KASI YAUA BODA BODA,SOMA HAPO KUJUA
DEREVA wa bodaboda mmoja amefikwa na mauti wilayani hapa juzi baada ya mwendokasi aliokuwa akiendesha kumfanya ashindwe kuimudu kwenye kona, kuanguka na kufa papo hapo huku mwingine akifariki baada ya kuligonga kwa nyuma lori lilikokuwa limeharibika.
Marehemu ametambuliwa kuwa ni mkazi wa kijiji na kata ya Ifwekenya wilayani Songwe mkoani Songwe: Tano Emmanuel (45).
Alifariki dunia kwa ajali hiyo iliyohusisha pikipiki yenye namba za usajili T612 CBT aina ya San Lig, imeelezwa na kwamba abiria wake wa jinsia ya kike alijeruhiwa.
Akizungumza jana na gazet hili, Kamanda wa Polisi mkoani humo, Mathius Nyange alisema ajali hiyo ilitokea saa moja usiku wa kuamkia jana na kwamba akiwa kwenye mwendo kasi, "dereva alishindwa kuimudu pikipiki yake kwenye kona na kujikuta akianguka na kufa papo hapo."
Kamanda Nyange alisema mbali na ajali iliyochukua uhai wa Emmanuel, pikipiki aina ya Fekon yenye namba T660 CXQ ikiendeshwa na Harusi Joseph (27), iligonga kwa nyuma lori lililokuwa limeharibika aina ya Scania namba T188 BAY na kusababisha kifo chake huku abiria aliyembeba akijeruhiwa pia.
Alisema dereva huyo wa bodaboda alikuwa amembeba abiria wa kuime ambaye alijeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili na kulazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Songwe kuendelea na matibabu.
Nyange alitoa wito kwa madereva wa bodaboda kuwa makini na kufuata sheria na alama za barabarani ili kukwepa vifo vinavyoweza kuepukika.
"Ndugu zangu wanahabari, madereva bodaboda wamekuwa hawafuati sheria za barabarani licha ya kuwapatia elimu mara kwa mara," alisema Kamanda Nyange.
Alisema askari kitengo cha Usalama Barabarani kuanzia sasa watafuatulia mienendo ya waendesha bodaboda ili kuhakikisha wanafuata sheria.

Reviewed by Unknown
on
15:48:00
Rating: 5