Home
/
Unlabelled
/
SATAKA LA KUKAMATWA MALOLI 600 YA TANZANIA,WIZARA YADAI HAINA TAARIFA,SOMA HAPO KUJUA
SATAKA LA KUKAMATWA MALOLI 600 YA TANZANIA,WIZARA YADAI HAINA TAARIFA,SOMA HAPO KUJUA
Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof.Makame Mbarawa
Dar es Salaam. Wizara imesema haina taarifa za kuzuiwa kwa malori 600 ya Tanzania nchini Zambia.
Akizungumzia suala hilo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Uchukuzi), Mhandisi Leornad Chamuriho amesema inawezekana wamiliki wa malori wanashughulikia suala hilo kupitia ubalozi wa Tanzania nchini Zambia pamoja na Wizara ya Mambo ya Nje Ushirikiano wa Afrika Mashariki Kikanda na Kimataifa.
Hata hivyo ameahidi kulifuatilia suala hilo ili kujua tatizo limetokana na nini.
Awali, akizungumza na waandishi wa habari, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Malori (Tatoa), Elias Lukumay amesema kukamatwa kwa malori hayo ni pigo kwa wamiliki kwa sababu wanahisi watafilisika hivi karibuni.
Lukumay amesema, pia Watanzania 1,200 ambao ni madereva na wasaidizi wao, wako nchini Zambia wakiwa wanalala kwenye malori kwa siku 60 sasa.
Hayo yametokea baada ya malori 600 ya Tanzania kuzuiwa nchini Zambia wakati yakitokea Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) yakiwa yamebeba magogo.
Zambia ilipiga marufuku usafirishaji wa magogo kwenda nje ya nchi, lakini DRC inaruhusu bidhaa hiyo kusafirishwa.
Jaffet Peter wa Kampuni ya Mature Logistics, amesema Zambia ni nchi rafiki na Tanzania lakini kitendo cha kuzuia malori yao kimewavunja moyo.
“ Zambia wameshindwa vipi kuwasiliana na Congo (DRC) wakati nyaraka ziko wazi zinaonyesha magogo ni ya Congo,” anasema.
SATAKA LA KUKAMATWA MALOLI 600 YA TANZANIA,WIZARA YADAI HAINA TAARIFA,SOMA HAPO KUJUA
Reviewed by Unknown
on
15:54:00
Rating: 5