MAKAMUWA RAIS AWATAKA WANAFUNZI NCHINI KUPENDA KUSOMEAA MASOMO YA SAYANSI KUFIKIA ADHAMA YA SERIKALI YA VIWANDA
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri wa Muungano ya Tanzania ,Samia Suluhu amewataka wanafunzi nchini kujibidisha katika kusoma masomo ya Sayansi ili kulisaidia Taifa linapoelekea sasa kwenye Tanzania ya Viwanda.
Pia,Amesema Taifa kutokuwa na watalamu wa sayansi litachangia
kurudisha adhama ya serikali kufikia malengo ya nchini kuwa na waatalamu wa
kuviendesha viwanda hivyo.
Makamu wa
Rais,ameyasema hayo leo Jijini Dar es
Salam wakati wa Maafali ya kidato cha sita kwa wanafunzi wanaosomeshwa na
Taasisi isiyo ya kiserikali inayotetea maendeleo kwa wanamke (WAMA).
Amesema kwa sasa licha ya serikali kujenga maabala takribani
shule zote za serikali pamoja na kuajiri walimu wengi wa sayansi kwenye shule za serikali basi ni
wajibu wa wanafunzi kusomea masomo ya sayansi.
Pia,Amewaomba wanafunzi hao wa kidato cha sita
kutumia fursa ya ukuaji wa mitandao kwa kupata maarifa badala ya kutumia mitandao hiyo kwenye mambo yasiyo faa katika
jamii ambayo amedai yatafifisha juhudi zao za kifikisha malengo yao
waliyojiwekea .
Kwa upande wake Mwenyekiti wa (WAMA) Mama Salma
Kikwete ambaye ni Mke wa Rais Mstaafu Jakaya Kikwete amesema Taasisi hiyo
itaendelea kuwasomesha wanafunzi wenye mazingira magumu ili wafiikie malengo ya
kulisaidia taifa.