MAPYA YAIBUKA KUPOTEA KWA BEN SAA NANE,JESHI LA POLISI NA KAMPUNI ZA SIMU ZAJIKANYAGA KWENYE TAARIFA YA SIMU YA SAA NANE,SOMA HAPO KUJUA
NA KAROLI VINSENT
WAKATI satata la Kupotea msaidizi wa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema,Ben Saanane likiwa bado linaumiza vichwa watu mbali mbali nchini huku wabunge wakitaka iundwe kamati maalumu ya kuchunguza kupotea kwa Msaidizi huyo wa Freeman Mbowe.
Mapya mengine yameibuliwa na Umoja wa Kizazi cha kuhoji nchini (UTG) kuhusu Mawasiliano ya simu ya Ben ya mwisho ambayo yanatajwa uwenda yakaliweka Pabaya Jeshi la Polisi nchini, baada ya kubainika taarifa iliyotolewa na jeshi la Polisi na Kampuni ya simu ambayo aliokuwa anatumia kujaa utata mtupu.
Akizungumzia utatau huo wa Taarifa hiyo wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam ,Mwenyekiti wa (UTG)Godlisten Malisa,amesema UTG unatilia shaka ukweli wa taarifa ya mawasiliano ya mwisho ulitolewa na Jeshi la Polisi kitengo cha Uhalifu wa mtandao (Cyber-Crime) umejaa makosa makubwa yaliojaa uposhaji,
Malisa ,Amesema Mawasiliano hayo ya polisi yanaonyesha kuwa Ben aliwasiliana mara ya mwisho kupitia simu yake mnamo tarehe 16/11/2016.
“Hii taarifa imeupotoshaji kwani taarifa zilizopo zinadai Ben aliondoka nyumbani kwake tarehe 18/11/2016.kwa mujibu wa mawasiliano yaliyowasilishwa na hao polisi yanaonesha kuwa Ben hakuwasiliana kabisa kwa muda wa siku mbali yaani tarehe 17 na 18 jambo ambalo UTG tunaamini sio kweli”Amesema Malisa.
Malisa ameendelea kuhoji kwa kusema Ben aliondoka nyumani kwake tarehe 18/11/2016 iweje mawasiliano yake ya mwisho yawe tarehe 16/11/2016? Huku akiohoji kwa simu mbili kabla ya ben kupotea je hakupigiwa simu kabisa.
“Yaani katika siku mbili hizo Ben hakutuma ujumbe wowote wa sms wala kutumiwa ?UTG tunatilia shaka kwamba huenda mawasiliano ya ben ya siku za mwisho (tarege 17 na 18)yamefishwa kwa sababu maalum’ameongeza Malisa.
Hata Hivyo ,Malisa amesema UTG kwa kushirikiana na Familiya ya Ben wamefuatilia mawasilano yaliyotolewa na Jeshi la Polisi kwa tarehe inayoishia 16 ,na kubaini namba zinazodaiwa ziliwasiliana na Ben kuwa namba hizo si za marafiki wake wala jamaa zake.
“Licha ya hizi namba tulizopewa kutozifahamu pia namba hizi za mwisho tumezibaini hazijawai kuwasiliana na Ben huko nyuma”
Malisa,amesema baada ya UTG kubaini utata huo wamelitaka jeshi la Polisi kuzichunguza namba hizo za mwisho zilizowasiliana na Ben ili wajulikane watu hao ni wakina nani?
Pia UTG umesema teyari wamewasilisha Malalamiko hayo rasmi kwa maandishi kwa Tume ya Haki na Binadamu na utawala bora ili tume hiyo imuagize Mkemia mkuu wa serikali ili ashirikiana na Mamlaka zingine wafukue miili ya watu 7 waliyoizika kando ya myo Ruvu wilayani Bagamoyo ili ifanyiwe vipimo vya vinasaba jambo wanalodai umoja huo itasaidia kwa ndugu wa Miili hiyo 7 ilioyozikwa kiinyeji ijulikane.