Zinazobamba

KUTEKWA NYALA MSANII ROMA MKATOLIKI,WASANII KIBAO WAONYESHA MASKITIKO,SOMA HAPO KUJUA

Sitomfahamu ya usalama wa Mwanamuziki wa Bongo Hipo Hop Ibrahim Mussa A.K.A, Roma yazidisha hofu kwa wanamuziki mbalimbali 
Fid Q
Nimeipokea hii HABARI kwa mstuko mkubwa.. sio tu kwasababu TONGWE ni moja kati ya wadhamini wetu wa #OpenMicThursday pia ni moja kati ya studio ambazo zimekua msaada mkubwa sana ktk kunyanyua vipaji na C E O @j_murder_tongwe amekua mstari mbele sana ktk kufanikisha hilo.. kinachonistua na kuninyima raha zaidi ni hili la hawa ndugu zetu akina @roma2030 @moni_centrozone Producer Belo na mlinzi kuwa hawajulikani waliko hadi hivi sasa.. ninaiomba MAMLAKA HUSIKA ya USALAMA itusaidie ili waweze kupatikana mapema na kuifutilia mbali ile hofu iliyotanda mioyoni mwa ndugu, jamaa na marafiki… mwisho namuomba MUWEZA WA VYOTE azifanyie wepesi familia za ndugu zetu waliopotelea kusikojulikana in sha Allah.
Professor Jay
Wakati sisi tunakosa Usingizi na kuendelea kupaza Sauti, Kuna wengine wameweka miguu juu wanaona hili haliwahusu na wengine wanakwenda mbali zaidi na kudiriki kusema hii ni KICK ya Muziki tu..
Narudia tena kuwaambia ndugu zangu WAKIMALIZANA NA SISI WATAKUJA KUMALIZANA NA NYINYI😭😭😭
#Bring Back our SOLDIERS Alive.
Vanessa Mdee
Wherever you are, God is Bigger than, Stronger than, Realer than all the other forces that be. Stay UP brother @roma2030 #VivaRoma #FreeRoma #FreeMoni roho inauma na nimetoka kumsikiliza mkeo redioni hajui hata ulipo sasa ndiyo nini 😡😡😡😡😠is this where we are at now? Ma studio yanavamiwa, watu wanakamatwa kama wanyama pori. Aaaarrrrgh
Diamond
Wakati mwingine natafakari sijui hata wapi tunaelekea… lla kwakuwa Mwenyezi Mungu ndio Mpangaji wa yote basi naamini hata hili litapita tu… Mwenyezi Mungu aipe nguvu familia ya @roma2030 na wanamziki wenzetu wote ambao hadi sasa haijajulikana walipo..
Nay wa Mitego
Siku nzima ya leo nimekosa raha kabisa, cjui Mshkaji wangu Yupo kwenye hali gani, mazingira gani.? Roma yuko wapi.?! Sim yake ukipiga inaita Kama kawaidi, Masege Whatsup zinasomwa, Sim hazipokelewi. Vyombo husika tunaomba mtusaidie, tunaitaji kujua ndugu zetu wako wapi.? Hatuwezi kukaa kimya.
Hivi kweli tumefikia huku.? Tunaenda wapi.? #FreeRoma✊🏿
#Wapo

Ray C
Nimeanza kuingiwa na woga,nafikiria mambo mengi Roma alipo Sasa,anafanywa nini na tatizo ni nini mpaka imekuwa hivi na masaa yanaenda hakuna jibu lililo kamili!!hisia mchanganyiko na zote sio nzuri….Nini kinaendelea?Tatizo ni nini??Sababu ni nini?Bado najiuliza sipati jibu………
AY
Vyombo husika vifanye uchunguzi wa haraka tujue hali za wasanii wenzetu wako kwenye hali gani..@romamkatoliki Mungu yupo pamoja nanyi awaepushie lolote baya.. @tongwerecords @j_murder_tongwe