SERIKALI YA MAGUFULI YAGEUKA CUBA YA AFRIKA,YAATOA MADAKTARI WAKE KWENDA KENYA,SOMA HAPO KUJUA
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
akisalimiana na Waziri wa Afya kutoka nchini Kenya Dkt. Cleopa Mailu
aliyefika Ikulu pamoja na ujumbe wake kwa ajili ya mazungumzo.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa
katika mazungumzo na Waziri wa Afya kutoka nchini Kenya Dkt. Cleopa
Mailu kuhusu Tanzania kupeleka madaktari 500 nchini Kenya, Ajira za
Madaktari hao zitatangazwa mara moja na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu na
zitawahusu Madaktari ambao hawajaajiriwa Serikalini(hawapo katika
utumishi wa umma au taasisi za serikali) waliomaliza mafunzo kwa vitendo
na ambao wamesajiliwa na Baraza la Madaktari la Tanganyika.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa
katika mazungumzo na ujumbe kutoka nchini Kenya uliongozwa na Waziri wa
Afya kutoka nchini Kenya Dkt. Cleopa Mailu Ikulu jijini Dar es Salaam.