MADAWA YA KULEVYA YAMTESA MTOTO WA KIKWETE,AFUNGUKA TENA KUHUSU KADHIA HIYO,SOMA HAPO KUJUA
Mbunge
wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete, amezungumzia suala la marafiki zake
kuhusishwa na biashara ya dawa za kulevya huku akisisitiza kwamba
wanaodaiwa kuwa ni marafiki zake sio bali ni watu anaokutana nao katika
maeneo anayotembelea.
Mbunge
huyo amezungumza hayo jana jijini Dar es Salaam baada ya kuhojiwa na
Mamlaka ya kudhibiti na Kupambana na Dawa za kulevya nchini, ambapo
alisema roho yake imesuuzika kwani jamii imeamini kwamba hahusiki kwa
namna yoyote ile na biashara hiyo haramu.
Ridhiwani alieleza kufurahishwa kwake baada ya kuhojiwa na Mamlaka hiyo nchini.
“Nashukuru
kwa kuhojiwa huku nimepata nafasi ya kueleza ukweli juu ya jambo hili
ambalo lilishaanza kuleta taharuki katika jamii, sasa umma umejua kuwa
siuzi wala sihusiki na dawa za kulevya, roho yangu imesuuzika,” alisema Ridhiwani.
Alisema
vita ya dawa ya kulevya ni kubwa na inapaswa kupigwa na kila mmoja ili
kuokoa kundi kubwa la vijana ambao wanaathirika kutokana na suala hilo
na kwamba kuhojiwa kwake kumemfanya awe na amani.
“Naunga
mkono vita hii ya dawa za kulevya nchini kwani itasaidia kurudisha
nguvu kazi inayopotea kutokana na matumizi ya dawa hizo za kulevya kwa
mzazi ambaye mtoto wake ameathirika na matumizi ya dawa hizo anajua
uchungu wake na hasara zake,” alisema Ridhiwani.
Aidha,
aliongeza kuwa jamii inapaswa kusimama kwa kauli moja ili kuliokoa
Taifa na nguvu kazi inayopotea ili Taifa liwe na vijana wanaojitambua na
kutimiza wajibu wao katika kulitumikia taifa.
Ridhiwani
alisema mchakato huo wa kupambana na dawa za kulenya nchini umekuwa
ukiwachanganya wananchi kwani haieleweki ni nani anayehusika na
kushugulikia suala hilo.
“Huu
mchakato umekua ukichanganya, kuna watu wanaitwa kwa Kamanda Sirro na
wengine wanaitwa kwa Kamishna Sianga (Rogers), mfano msanii Vanessa Mdee
ambaye ameitwa kwa Kamanda Sirro badala ya kwa Kamishna Sianga,” alisema Ridhiwani.
Alisema
watu wanahoji kwanini wengine watangazwe hadharani na wengine kuitwa
kimya kimya na ameongeza kuwa ni vyema mamlaka zikajipanga ili
kufanikisha vita hii na kufikia malengo yake ya kumaliza tatizo la dawa
za kulevya nchini