WABUNGE WAIBANA SERIKALI BUNGENI,SOMA HAPO KUJUA
Wabunge wameitaka Serikali kutoa maelezo ya dola 300
milioni za Kimarekani (sawa na Sh570 bilioni) zilizotolewa na wahisani kwa
ajili ya kusaidia miradi ya afya, lakini hazijatumika.
Fedha hizo zilitolewa na Global Fund kwa ajili ya
kugharamia miradi ya Ukimwi, malaria na kifua kikuu (TB) na zinatakiwa hadi
kufikia Desemba mwaka huu ziwe zimeshatumika.
Mjadala huo ulizuka jana katika semina ya wabunge wa
kamati tatu za Bunge kuhusu afya ya wanawake, watoto na vijana iliyoandaliwa na
Umoja wa Mabunge ya Dunia (IPU) na Bunge la Tanzania.
Semina hiyo ilishirikisha Kamati ya Bajeti, Huduma
na Maendeleo ya Jamii na ya masuala ya Ukimwi.
Akizungumza katika semina hiyo, mbunge wa viti
maalumu (Chadema), Suzan Lyimo alisema bila kuwa na bajeti ya kutosha, malengo
ya pambano dhidi ya Ukimwi hayawezi kufikiwa.
“Tunasikia kuna wadau wengi waliokuwa
wanasaidia eneo hili wamejiondoa. Nataka kufahamu wanasemaje kuhusu hili?” alihoji.
Akijibu hoja hiyo, Marianna Balampama kutoka Kundi
la Washirika wa Maendeleo (DPG), alisema wafadhili hawajajitoa kusaidia miradi
hiyo. Alisema wafadhli hao kama Marekani na Global Fund wanaendelea kutoa
misaada.
Hata hivyo, alisema muda wa dola 300 milioni za
Kimarekani zilizotolewa na Global Fund unakaribia kuiisha, lakini
hazijatumika.
Alisema kutokana na masharti mapya ya Global Fund,
muda wa kutumika ukimalizika, kama hazijatumika hutakiwa kurudishwa.
Hali hiyo iliwafanya wabunge wengine kuanza kuguna
na wengine kunong’ona. Kutokana na maelezo hayo, Deogratius Rutatwa, ambaye ni
ofisa Mtendaji Mkuu wa Baraza la Watu Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (Nacopha),
aliiomba Serikali kuchukua hatua za haraka ili fedha hizo zisirudishwe.
Hata hivyo, Dk Nemes Irya kutoka Shirika la Afya
Duniani (WHO) aliwatoa hofu wabunge kuwa fedha hizo haziwezi kurudi kwa
wafadhili.
“Huwa fedha hizi zinakuja kwa
mafungu kama tunavyotekeleza miradi,” alisema.
Akijibu hoja hiyo, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu
alisema Serikali ilikuwa na mazungumzo na Global Fund ya jinsi ya kutumia kiasi
hicho cha cha fedha hizo katika kuboresha miundombinu. Waziri Ummy alisema
ameiam- bia Global Fund kuwa Serikali inataka iwe na uamuzi kwa asilimia 15 ya
fedha zinazotolewa.
“Mwaka huu nimewambia Global Fund, kati
ya hizo Dola 380 milioni za Kimarekani mnazotupatia, asilimia 15 nizitenge
mimi. Niamue tunazitumiaje, wasitu lazimishe tuzitumie kwaajili ya Ukimwi na
malaria tu, bali nizitumie kuboresha mifumo.” Ummy Mwalimu