TECNO MOBILE YASHINDA KAMPENI BORA ,YAPEWA TUZO YAKE,SOMA HAPO KUJUA
A
Kampuni inayoongoza kwa mauzo ya simu nchini
Tanzania, TECNO MOBILE imefanikiwa
kushinda tuzo za Tanzania
leadership Awards zilizofanyika mwishoni
mwa wiki Jijini Dar es salaam.
Katika mchakato wa tuzo hizo
zilizoandaliwa na Purple cow media,
Tecno iliingia katika tatu bora ikiwa
inashindana na kampuni mbili kubwa nchini Tanzania, kampuni ya mawasiliano ya
simu TIGO na kampuni ya vinywaji TBL ,
zote zikiwa katika kitengo cha kampeni
bora MITANDAO YA Kijamii ya mwaka katika
mitandao ya kijamii.
Tecno waliingia katika kinyang’anyiro
kupitia kampeni yao ya simu maarufu ya
TECNO CAMON C9, katika kampeni iliyoshika hisia za watumiaji wengi wa mitandao ya kijamii kutokana
na kuwapa nafasi watumiaji wa simu
kupiga picha kutokana na maelekezo
yaliyokua yanatolewa na account za mitandao ya kijamii za kampuni,
washiriki washindi walipewa zawadi
za aina mbalimbali zikiwemo simu
za TECNO CAMON C9.
Tecno imekua kampuni ya kwanza ya simu
kushinda katika kategori hiyo ya kampeni bora ya mwaka ya mitandao ya kijamii kutokana na uwezo wake
mkubwa uliojidhihirisha kwa kuwapa nafasi kubwa watumiaji wa mitandao na wateja
wake kufikisha matzo yao na kusaidiwa lakini pia wateja kuongea na watu
mbalimballi maarufu kama Salma Jabir, Hamisa Mobeto pamoja na Idriss Sultani
huku zawadi kemkem zikitolewa kwenda kwa watumiaji wa mitandao waliofwata TECNO
mobile katika mitandao.
Jamii ya Kitanzania itaendelea kufaidika na mitandao ya kijamii kupitia
kampuni kubwa ya Tecno Mobile wakifanya
matukio mbalimbali ikiwemo kampeni mpya
iliyopata umaarufu ya KAMA MBELE washindi wakipata nafasi ya kwenda
kushudia mchezo wa mpira wa miguu katika jiji la Manchester wakiwa na
mchekeshaji Idris Sultan, pamoja na Kampeni UPENDO inayowataka watumiaji kuweka
picha au video mitandao wakisema upendo kwao ni nini na video/picha bora itampa
nafasi mshiriki kuchaguliwa kwenda kusheherekea siku ya wapendao katika hotel
kubwa Nchini.