TAARIFA MUHIMU KUTOKA JWTZ KUHUSU ASKALI WAKE KUUA KONDAKTA,SOMA HAPO KUJUA
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania
limesikitishwa na taarifa iliyotolewa na gazeti la Tanzania Daima toleo Nambari
4438 la tarehe 28 Januari 2017, Habari leo la tarehe 29 Januari
2017 na baadhi ya vyombo vya habari vikihusisha mauaji ya kondakta wa daladala
na Wanajeshi Mkoani Tanga.
Tunapenda kuwataarifu wananchi kwamba kwa
mujibu wa jeshi la polisi watuhumiwa wanaoshikiliwa na Jeshi hilo ni wanne
(4),mmoja kati yao ni Mwanajeshi ambaye ni mzazi wa msichana anayetuhumiwa
kusababisha tukio hilo.
Hivyo Mwanajeshi huyo anashikiliwa kwa ajili ya
kulisaidia Jeshi la Polisi katika uchunguzi kwa kuwa tukio hilo lilifanyika
nyumbani kwake.
Hakuna Wanajeshi waliohusika katika tukio hilo kama
ilivyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari, kambi za Jeshi wanaishi
Wanajeshi pamoja na familia zao hivyo kuhusisha moja kwa moja mauaji hayo na
Wanajeshi mkoani Tanga ni kuupotosha umma.
Wito unatolewa kwa vyombo vya habari kuripoti habari
zenye ukweli.Habari zisizo za kweli zinapotosha umma na kujenga taswira potofu
kwa wananchi dhidi ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.
Imetolewa na Kurugenzi
ya Habari na Mahusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
S.L.P 9203,
Dar es Salaam,
Tanzania.
Kwa Mawasiliano zaidi: 0756-716085