SHIRIKA LA LSF YAWASIFU WABUNGE KWA KUPITISHA MSWAADA HUU,SOMA HAPO KUJUA
Afisa kutoka LSF,
Bi. Fortunata Kitokesya akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) wakati wa
akielezea namna Shirika hilo linavyofanya kazi hapa nchini katika kusaidia
misaada ya kisheria hasa kwa wanawake.
|
NA KAROLI VINSENT
WAKATI Bunge la Jamhuri wa Muungano la Tanzania
likiwa limepitisha mswaada wa huduma ya sheria wa mwaka 2016,
Wadau wa sheria nchini wameusifu mswaada huo kwa
kusema utasaidi wasaidizi wasaidizi wa sheria kufanya kazi kwa uhuru pamoja na
kutambulika kisheria tofauti na mwanzo.
Fortunata Kitokyesya ambaye ni Afisa mradi wa
Taasisi isiyokuwa ya kiserikali inayohusika na utoaji wa msaada wa kisheria
'LSF' wakati wa taasisi hiyo ilipokuwa inatoa msaada wa kopyuta mpakato kwa
wasaidizi mbalimbali wa sheria walioko mikoa mbali ili waweze kutoa msaada kwa
haraka kwa jamii,
Ambapo amesema wamepokea kwa moyo mmoja ujio wa
msaada huo ,ambao wanadai utawasaidia katika kufanya kazi kwa uhuru.
Amesema mswaada huo pamoja na mambo mengine umetoa
ruhusa kwa wasaidizi wa sheria kutambulika kisheria tofautisha na hapo mwanzo
ambapo wasaidizi hao walionekana ni matapeli.
Amebainisha kuwa kwa sasa wasaidizi wa sheria
walioko vijijini watafanya kazi ya kuwasaidia wananchi wanaoitaji msaada wa
kisheria kwa haki.
Dk. Benson Bana mjumbe wa Bodi ya LSF akizungumza na waandishi wa
Habari (Hawapo pichani) wakati akizungumzia tukio hilo.
|
Kwa upande wake Mhadhili mwandamizi kutoka chuo
kikuu cha mlimani UDSM Dokta,Bensoñ Bana ambaye ni Mjumbe wa Bodi ya LSF ameusifu mswaada huo huku akimtaka
Rais John Magufuli kuusaini haraka na kuwa sheria ili uweze kuwasaidia
kaya masikini ambayo ilikuwa inahangaika kukosa haki.
Pia, Dokta Bana amemtaka Waziri wa Katiba na
Sheria,Dokta Harrison Mwakyembe kuharakisha uandikaji wa Kanuni mara baada Rais
Magufuli kuusaini mswaada huo ili uanze kutumika haraka