SERIKALI YAGUSHWA NA SHIRIKA LA FEMINA,SOMA HAPO KUJUA
WIZARA
ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi imezitaka shule za sekondari
na msingi nchini kuanzisha club za maadili ili kuzuia mmomonyoko wa maadili
ndani ya jamii lakini pia kujenga uzalendo ambao umeanza kutoweka miongoni mwa
vijana wa Kitanzania.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam
leo kwenye mkutano wa mwaka wa
vijana ulioandaliwa na shirika lisilo la
kiserikali la FEMINA HIP Kaimu Kamishna wa Elimu nchini kutoka wizara hiyo Mwalimu Nicholaus Bureta amesema kuwa mpaka
sasa wizara imeshaanzisha club za
kupambana na rushwa shuleni ili kutoa muongozo bora kwa wanafunzi na kuzalisha
vijana wenye kuchukia rushwa na kuzingatia maadili.
Aidha, Mwalimu Burete ametoa wito kwa wadau wote wa
elimu nchini wakiwemo wazazi na walezi kuhakikisha kwamba wanawajenga watoto
wawo katika misingi bora ili Taifa liweze kuzalisha vijana wenye uzalendo wa
kupenda nchi na kushirikiana na jamii katika kuleta maendeleo.
Katika hatua nyingine kaimu kamisha wa elimu
nicholus Burete amezungumzia juu ya matokeo ya mtihani wa taifa wa kidato
channe yaliyotoka jana ambapo shule sita za mkoa wa dare s salaam zimeshika
nafasi ya mwisho na kuufanya mkuo huo kuwa wa mwisho kitaifa, amesema kuwa wizara
inatambua suala hilo hivyo inajiandaa kukaa pamoja na mamlaka ya mkoa huo
ili kuangalia kitu kilichosababisha shule hizo kufanya vibaya.
Calvin Muhagama ni mwalimu kutoka shule ya Sekondari
ya Aron harris iliyopo Pugu Kichangani Jijini Dar es Salaam amebainisha kuwa
vipo vitu mbalimbali vinavyochangia baadhi ya shule kufanya vibaya ama mkoa
Fulani kufunya vibaya ambapo amevitaja vitu hivyo kuwa ni pamoja na sera ya
elimu nchini kukandamiza walimu pamoja
na uwepo wa miundombinu mibovu ya utendaji kazi kwa walimu.