Zinazobamba

MTANZANIA ADAKWA NA MADAWA YA KULEVYA NCHINI INDIA,SOMA HAPO KUJUA

 
Kushoto ni Mtanzania aliyejulikana kwa jina la Pamela David Kirrita (41) akiwa  na mwanamke mwingine raia wa Zambia Thelma Mkandawire (38) wakiwa  mbaroni kwa tuhuma za kukutwa na kilo 4 za madawa ya kulevya aina ya  cocaine katika hoteli moja kusini mwa jiji la New Delhi, India.

Naibu Mkurugenzi Mkuu wa kikosi cha kupambana na madawa ya kulevya cha New  Delhi (NCB) Rajinder Pal Singh amesema watuhumiwa walikamatwa katika hoteli iliyopo eneo la Mahipalpur jana Februari 4, 2017.

“Baada ya kupata taarifa kutoka vyanzo vyetu, timu yetu ikatega mtego kwa  Mkandawire aliyewasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Indira Ghandi  akitokea ughaibuni akiwa na mzigo huo.
“Baada  ya kuchekiwa uwanjani pale aliondoka na taxi hadi hotelini. Timu yetu ilimfuatilia na kumuona mara alipofika hotelini akakutana na Pamela  David Kirrita aliyekuwa aupokee huo mzigo”, alisema Mkurugenzi wa NCB  tawi la New Delhi.

Amesema walipohojiwa Kirrita alibainisha kuwa alikuwa akiishi katika hoteli moja katika kitongoji kiitwacho Vasant Kunj tokea  Januari, na kwamba  alikuwa na mawasiliano na mtu mwingine raia wa kigeni ambaye ndiye  angempasia mzigo baada ya kuuchukua toka kwa Mkandawire. 

Polisi wanasema mzigo ulifichwa kwenye uwazi wa begi la safari, na kwamba  Mkabdawire aliwahi kukamatwa nchini Pakistani mwaka 2015 na kukaa  mahabusu kwa zaidi ya miezi sita, huku Pamela akikiri kutembelea India  zaidi ya mara sita tokea mwaka 2006.




Kwa sheria za India, mshtakiwa atayekutwa na hatia ya madawa ya kulevya  yaliyokuwa ya kibiashara ni kifungo cha kati ya miaka 10 ama 20 gerezani na faini ya Rs 1 lakh (sawa na dola za Kimarekani 15,000) ama Rs 2  lakhs (dola 3000).