WAZIRI KAIRUKI NAYE AHAMIA RASMI MKAONI DODOMA,SOMA HAPO KUJUA
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi
wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki amezindua rasmi safari ya
awamu ya kwanza kwa kuaga msafara wa
magari yaliyobeba vifaa vya Ofisi vya kundi la kwanza
la watumishi wa ofisi hiyo kuelekea Dodoma.
Akizungumza
katika uzinduzi huo Mhe. Kairuki alisema
umefika wakati wafanyakazi wa Serikali kuanza safari ya kuamia makao makuu
Dodoma ili kutimiza ahadi iliyotolewa na
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.John Pombe la watumishi wa ofisi hiyo kuelekea Dodoma.
Magufuli wakati wa Maadhimisho ya kumbukumbu ya siku ya Mashujaa.
“Kufuatia agizo la Mheshimiwa Rais, Mheshimiwa Waziri Mkuu kama kiongozi na mratibu wa shughuli za Serikali alihamia Dodoma Mwezi Septemba 2016,Wizara nyingine zimeendelea na maandalizi ya kutekeleza azma hii ya
serikali, nami leo napenda kutumia fursa hii kuuarifu umma wa
watanzania kuwa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora imekamilisha maandalizi ya kuhamia Dodoma na hivi punde vifaa vya kundi la kwanza vitaondoka kwenda Dodoma”,Aliongeza Mhe. Kairuki.
Amesema katika kundi la kwanza jumla ya watumishi 87 watahamia Dodoma na litahusisha uongozi wa Juu wa Wizara ukiwajumuisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Katibu Mkuu na
Naibu Katibu Mkuu na Baadhi ya Wakurugenzi, Wakurugenzi Wasaidizi, Maafisa Waandamizi na Watumishi wengine.
Katika hatua nyingine Mh. Kairuki alisema wale wote wanaohitaji kukutana na Waziri,Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu wake wafike katika Ofisi zilizopo Dodoma na kwa
masuala yote yanayohusuu Sera na Sheria za Utumishi wa Umma na Utawala wa Utumishi wa Umma kwa Ujumla yatatekelezwa Mjini Dodoma lakini.
Aidha masuala ya Mishahara,Uendelezaji rasilimali watu,Ukuzaji maadili,Anuai za jamii,Uchambuzi ushauri na Utendaji kazi na Huduma ya teknolojia ya habari na mawasiliano yataendelea kushughulikiwa na ofisi ya Dar es
Salaam.
Alisema Ofisi yake itafunguliwa Rasmi Mjini Dodoma Tarehe
30 Januari 2017 na itakuwa katika Jengo la College of Humanities and Social Sciences katika eneo la Chuo Kikuu cha Dodoma kama makao yake ya muda mpaka hapo itakavyoelezwa vinginevyo.