TRUMP AKASIRIKA SASA,AMTIMUA KAZI MWANASHERIA MKUU,SOMA HAPO KUJUA
Rais
wa Marekani, Donald Trump amemfuta kazi Kaimu Mwanasheria Mkuu wa
Marekani, Sally Yates saa chache baada ya kiongozi huyo kuwaagiza
Mawakili kutotetea uamuzi wa kuwawekea vikwazo vya kuingia Marekani raia
wa nchi saba zenye waislamu wengi.
Sally
Yates aliyeteuliwa na Rais Obama alisema kuwa alitoa agizo hilo kwa
Mawakili sababu haamini kama zuio la raia kuingia Marekani ni halali.
Rais
Trump Ijumaa alitia saini amri inayozuia raia kutoka Somali, Sudan,
Libya, Yemen, Iran, Syria na Iraq kuingia nchini Marekani ambapo zuio
hilo ni la siku 90.
Maandamano
yamezuka maneneo mbalimbali ya Marekani huku wakipinga zuio hilo.
Wanadiplomasia wamesema kuwa zuio hilo huenda likasababisha hatari zaidi
kwa usalama wa Marekani.
Aidha, baadhi wamehoji kwanini zuio limewekwa kwa nchi hizo saba wakati kwa miaka ya hivi karibuni hakuna raia wake aliyehusika na ugaidi nchini Marekani?
Aidha, baadhi wamehoji kwanini zuio limewekwa kwa nchi hizo saba wakati kwa miaka ya hivi karibuni hakuna raia wake aliyehusika na ugaidi nchini Marekani?
Rais
Trump amevikosoa vyombo vya habari vinavyopotosha kuwa zuio hilo ni
kwa Waislamu pekee. Rais Trump amesisitiza kuwa zuio hilo ni kwa raia
wote wanaotoka katika nchi hizo hata kama si Waislamu.
Trump
alisaini amri hiyo katika kile alichosema kuwa ni kuzuia watu wenye
misimamo mikali kuingia nchini Marekani ikiwa ni hatua za kuimarisha
ulinzi na usalama.