CUF YA LIPUMBA YAIJIBU CUF YA MAALIM SEIF,NI KUHUSU FEDHA ZA RUZUKU,SOMA HAPO KUJUA
Mkurugenzi wa Fedha na Uchumi (Taifa) wa Chama cha Wananchi (CUF), Thomas
D.C Malima (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa
habari Makao Makuu ya Chama hicho jijini Dar es Salaam leo kuhusu ruzuku
ya chama hicho iliyopokelewa kupitia akaunti namba 2072300456 ya Benki
ya NMB Tawi la Temeke. Kulia ni Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi, Mneke
Jafar na Katibu Jumuiya ya Wanawake (JUKE), Salama Masoud.
NA KAROLI VINSENT
Siku moja kupita baada Bodi ya udhamini la chama cha
wananchi cuf kutangaza kuzifunga akaunti zote za wilaya nchi nzima za chama
hicho kwa madai ya akaunt hizo zinatumika kuiba ruzuku za chama.
Nao baadhi ya viongozi wa Cuf ambao wanamuunga mkono
mwenyekiti anayetambulika na ofisi na msajili wa vyama vya siasa,Profesa
Ibrahimu Lipumba wameibuka na kusema Bodi hiyo aitambuliki kisheria kutokana na
mda wake kuisha kikatibu.
Pia,viongozi hao wamekanusha tuhuma za ruzuku
kuibiwa kwa kudai kuwa ruzuku iliyotolewa na msajili imetumika kujenga
chama hicho kwenye uchaguzi mdogo uliomalizika hivi karibuni.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini dar es
salaam,mkurugenzi wa fedha wa chama hicho,Thomas Malima
amesema chama hicho hawalitambui bodi iliisha tangu mwaka 2015.
Amesema kwa mujibu wa ibara 98 kifungu cha 1 inasema
kutokuwa na bodi ambayo itadumu miaka mitano ,hivyo bodi hiyo iliundwa 2010 na
mwisho wake ni 2015.wanashangaa hatua ya bodi hyo kutoa makatazo.
Hata hivyo, chama hicho kimetoa ufafanuzi wa
mgawanyiko wa ruzuku kwa kusema ruzuku iliyotolewa na chama hicho ilitumika
kukijenga chama cha Cuf.
Malima akichanganua mgawanyiko huo amesema chama
hicho kimepokea milioni 369.366.671 kupitia Akounti 2072300456
ya The civic United Front Cuf kwa wilaya ya temeke.
Amedai sehemu ya fedha milioni 66.300.000 zimetumika
kupeleka ruzuku kwa wilaya ya chama hicho huku kilichobakia kilitumika kutumika
kwenye uchaguz mdogo.