TIZAMA SHULE BORA ZILIZOFANYA VIZURI,NA ZILIZOSHIKA MKIA,PAMOJA NA WANAFUNZI BORA KWENYE MATOKEO YA KIDATO CHA NNE,SOMA HAPO KUJUA
Leo January 31 2017 Baraza la mitihani Tanzania NECTA limetangaza matokeo ya kidato cha nne ‘CSEE 2016’.
Hapo chini kuna orodha ya shule 10 bora kitaifa na shule 10 zilizoshika mkia
Wanafunzi 10 bora waliofanya vizuri hawa hapa
Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) limetangaza
matokeo ya kidato cha nne mwaka 2016 ambapo umefaulu wa jumla umeongezeka kwa
2.56% kutoka 67.53% mwaka 2015 hadi 70.09% mwaka 2016.
Katibu Mtendaji wa barza hilo, Dkt Charles Msonde
amesema kati ya wanafunzi 408,372 waliofanya mtihani, jumla ya wanafunzi
277,283 wamefaulu, wakiwemo wasichana 135,859 sawa na asilimia 67.06 na
wavulana 141,424 sawa na asilimia 73.26.
Kwa upande wa watahiniwa wa shule, Dkt Msonde
amesema kuwa 244,762 sawa na asilimia 70.35 ya waliofanya matihani wamefaulu
ikilinganishwa na wanafunzi 240,996 sawa na asilimia 67.91 waliofaulu mwaka
2015.
Kwa upande wa ubora wa ufaulu, amesema watahiniwa wa
shule wenye ufaulu mzuri wa Daraja la kwanza hadi la tatu ni 96,018 sawa na
asilimia 27.60.
Kwa upande wa masomo, amesema ufaulu katika masomo ya History, Geography, Kiswahili, English Language, Basic Mathematics, Physics, Biology, Commerce na Book keeping umepanda kwa kati ya asilimia 0.12 na 8.08 ikilinganishwa na mwaka 2015.
Somo lililoongoza kwa ufaulu ni Kiswahili ambapo asilimia 77.75 wamefaulu na somo la mwisho ni Basic Maths ambalo asilimia 18.12 ya watahiniwa wa shule wamefaulu.
Kati ya wanafunzi 10 bora kitaifa, wanafunzi 5 ni wasichana na 5 ni wavulana wakiongozwa na Alfred Shauri kutoka Feza Boys ya Dar es Salaam
Kati ya shule 10 zilizofanya vibaya kitaifa, shule 6 zinatoka katika mkoa wa Dar es Salaam wakati shule iliyoongoza ikiwa ni Feza Boys ya Dar es Salaam. Pia katika shule kumi bora kitaifa, hakuna shule ya serikali
Mkoa wa Njombe umeongoza katika mikoa 10 iliyofanya vizuri zaidi kitaifa ukifuatiwa na Iringa, Kagera, Kigoma na Kilimanjaro huku halmashauri za Bukoba Mjini, Njombe, Kakonko, Kahama na Wang'ing'ombe pia zikiibuka vinara

A