SERIKALI YA MAGUFULI YAMUAMULIA MBUNGE FREEMAN MBOWE,BAADA YA BILLCANAS YAAMUA KUMFUTA KIJIJINI KWAKE,SOMA HAPO KUJUA
Miezi takribani mitano iliyopita tangu aondolewe
Billcanas, siku moja tangu Serikali imzuie asiendelee na shughuli za kilimo
katika shamba lake, Mwenyekiti huyo wa Chadema amepewa siku 14 awe amelipa kodi
inayokadiriwa kufika milioni 13.5, ya hoteli yake ya Aishi iliyoko Machame
Mkoani Kilimanjaro.
Uamuzi huo mpya wa Serikali wa Wilaya ya Hai, Mkoani
Kilimanjaro,umefikia hatua hiyo ikiwa ni siku moja baada ya Mkuu wa Wilaya hiyo
Gellasius Byakanwa, kutangaza kusitisha shughuli za kilimo katika shamba la
Veggies analomiliki Mbowe kutokana na kile kilichosema lipo ndani ya chanzo cha
maji.
Byakanwa amesema kuwa Serikali ya awamu ya Tano
imelenga kukusanya mapato ili iweze kutekeleza majukumu yake ikiwamo kutekeleza
ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM).
“Hatuwezi kufikia malengo ya ukusanyaji mapato yetu
ya ndani kama kuna wafanyabiashara wakubwa kama huyo wanakwepa kulipa kodi, na
tena kwa kipindi chote hicho ameshindwa kuleta hali ya mauzo yake ambayo
yataweza kujulikana kiasi anachostahili kulipa kodi,”amesema Byakanwa.
Hata hivyo Mkuu huyo wa Wilaya amemshutumu Mbowe kwa
kufanya uharibifu wa mazingira kwa kuvuna miti ya asili bila kibali cha mkuu wa
Wilaya kulingana na uamuzi wa Kamati ya ushauri ya Mkoa (RCC) pamoja na kuvuta
maji kwa kutumia mashine kinyume na kibali na taratibu za utumiaji wa maji
mfereji.