WEZI WA FEDHA ZA RUKUZU ZA CUF,MAALIM SEIF AMLIMA BARUA KALI GAVANA,SOMA HAPO KUJUA
Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim
Seif Sharif Hamad, amemwandikia barua Gavana wa Benki ya Tanzania (BoT),
Profesa Beno Ndulu ili achukue hatua za kulishughulikia sakata la fedha za
ruzuku zinazodaiwa kukwapuliwa na CUF upande wa Mwenyekiti anaetambuliwa na
Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba.
Maalim Seif ameandika barua hiyo yenye kumbukumbu
namaba CUF/HQ/AKM/003/017/01 na nakala zingine kuzituma kwa mamlaka mbalimbali.
Katika barua hiyo kwa Profesa Ndulu, Maalim
ameamabatanisha kumbukumbu ya miamala ya fedha ilivyofanyika, pia amesema kuwa
chama hicho kinaendelea na taratibu za kukamilisha hatua za kisheria ili
kuwafikisha mahakamani wahusika wote walioshiriki katika kuchukua fedha
hizo, akiwapo Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji Francis Mutungi.
Amesema kuwa, Mutungi atakuwa na kesi ya pili na
atashtakiwa kutokana na madai ya kushirikiana na walalamikiwa wale wale wa
kufungua akaunti mpya ili wapewe ruzuku.
Aidha, amesema Jaji Mutungi amefanya hivyo huku
akifahamu fika kuwa kuna kesi ya msingi iliyopangwa kusikilizwa Februari 2,
2017 mbele ya Jaji Kihiyo.
“Gavana baada ya Muhtasari huo, kwa masikitiko
makubwa leo nakuandikia barua hii kukujulisha kuwa njama za kuiba fedha za
ruzuku ya CUF Chama cha Wananchi zimefanikiwa kwa kufanya muamala
wa jumla ya shilingi 369,378,502.64 toka kwa Msajili wa Vyama vya Siasa nchini
kwenda akaunti namba 2072300456 ya NMB tawi la Temeke januari 5 mwaka
huu,”amesema Maalim.
Hata hivyo, hivi karibuni CUF upande wa Maalim Seif
ulilalamikia hatua iliyochukuliwa na Jaji Mutungi kuwapa CUF upande wa Profesa
Lipumba zaidi ya shilingi milioni 360 za ruzuku