SAKATA LA MGOGORO NDANI LA KANISA LA AGLIKANA,ASKOFU MOKIWA AIBUKA NA KUFICHUA MAZITO,SOMA HAPO KUJUA
NA KAROLI VINSENT
MKUU wa kitivo cha sheria kutoka chuo cha Mlimani (UDSM)_Profesa
Parama Kabudi ametajwa kuwa ndio kinara anayesabibisha migogoro ndani ya Kanisa
Aglikana nchini baada kutajwa kuhusika kumshauri vibaya Askofu Mkuu wa Kanisa
hilo Dk Jacob Chimeledyaili achukue maamuzi ya kumvua uaskofu Mkuu wa
Dayosisi ya Dar es Salaam Dk Valentine Mokiwa.
Mbali na
Msomi huyo .pia vyombo vya serikali
yakiwemo magari ya umma na jeshi la Polisi nalo limehusishwa na mgogoro huo,
Sanjari na watu hao pia Kanisa la Aglikana la
magomeni jijini hapa nalo pia limetuhumiwa katika kutengeneza mgogoro huo.
Hayo yameibuliwa leo jijini hapa na Askofu Dk Mokiwa
wakati wa mkutano na waandish wa habari
ili kuzungumzia maamuzi yaliotangaza mkuu ya kumvua uaskofu wake kutokana
tahuma mbali mbali ikiwemo matumizi mabaya ya fedha.
Amesema Amesikishwa maamuzi hayo huku akisikitiza watu wanaoumshauri askofu mkuu huku akimtaja kwa majina mwanasheri Parama Kabudi ndio amekuwa kinara wa kuanzisha migogoro mara kwa mara.
Amesema kabudi amekuwa akitoa ushauri mbovu kwa
askofu mkuu jambo analosema aliendani na hadhi yake ya uanasheria alionao.
“'Mara kwa mara serikali imekuwa ikionya kuhusu
mgogoro ndani ya kanisa letu,na mgogoro anasabisha huyu mtu kutokana na ushauri
wake ambao askofu mkuu anauchukua ambo ni hatari kwa kanisa”Amesema Mokiwa.
Mokiwa amelitaja kanisa magomeni ndio limekuwa likihusika katika kuteneza migogoro amedai kuwa padri wa kinisa hilo wamekuwa wakitengeneza tuhuma juu yake ambazo hazina ukweli
Kuhusu mali za serikali kutumika kwenye kutengeza
mgogoro huo,amesema hakuna mahali popote ambapo yeye amefuja mali za kanisa
huku akidai watu wasiponda kazi ya
injiri wamekuwa mara kwa mara wakimtengenezea skendo hizo ambapo hazina ukweli.
Askofu Mokiwa pia ameonyesa masikitiko yake kwa kile anachodai serikali imehusika kutengeza mgogoro huo baada ya kutaja gari aina ya Toyota landgrucer yenye namba STK 2940 Kutoka mkoa wa Singida zimehusika katika kuwapakia watu anawoita ni watengeneza mgogoro wa kanisa hilo.
Mbali na Garà hilo,pia mtumishi huyo wa kiroho
amewatuhumu askari wa jeshi la polisi ambapo anadi polisi hao walivamia kikao
cha kanisa pamoja na askofu mkuu kanisa bilo kama kunaugomvi .
KUHUSU TUHUMA ZA KUUZA MALI ZA KANISA
Mukiwa amesema tuhuma hzo hazina ukweli na zimetengengenezwa na watu amboa aliwafukuza upandri kutokana na tuhuma mbali za kanisa.
Mukiwa amesema tuhuma hzo hazina ukweli na zimetengengenezwa na watu amboa aliwafukuza upandri kutokana na tuhuma mbali za kanisa.
“Ule waraka tuliupitia na kubaini kuwa hauna baraza
za nyumba ya maakofu, wala hauna baraka za halmashauri ya kudumu na Sinodi ya dayosisi,”
alisema na kuongeza kuwa maamuzi ya kumvua uaskofu Dk Mokiwa yamefanywa na
askofu mkuu wa Tanzania kwa kushinikizwa na watu wachache aliowavua vyeo na sio
vikao vya kanisa.
Lakini alipoulizwa askofu mokiwa swali na waandishi
wa habari kuhusu kudaiwa kutelekeza Nyumba iliyopo Osyterbay na nyingine
iliyopo Upanga jijini Dar alisema kuwa nyumba hizo siyo za kwake bali ni mali
ya kanisa na sio zimetelekezwa bali zipo katika hatua ya ujenzi wa nyumba za
kisasa.
Dkt. Mokiwa amesema kuwa tuhuma zote zilizotolewa
dhidi yake ni za kumchafua na kulenga kumchonganisha dhidi ya waumini
wake na wanaofanya hivyo ni wale waliokiuka miiko ya kanisa akawavua
vyeo, huku akiwataja kuwa ni Mchungaji John Mhina, mchungaji Johnson
Chinyong’ole wa kanisa la Newala na Paul Mtweve aliyemtaja kuwa alikuwa katibu
wa uinjilisti Dayosisi ya Magomeni.
Alisema kuwa hao ndio wavunjifu wa amani katika
dayosisi hiyo ndio maana akaamua kuwatimua na hivi sasa wamerudi kivingine ndio
hao hao ambao wamesababisha mgogoro huu unaojitokeza hivi sasa.