SAKATA LA KUUNGUA UWANJA WA NDEGE WA MWALIMU NYERERE,WAZIRI WA MAGUFULI AJITOSA,SOMA HAPO KUJUA
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (katikati),
akiwa na viongozi mbalimbali wakiwemo wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Julius Nyerere (JNIA) wakati akitoka kukagua chumba namba cha
kuhifadhia mizigo kilichoungua moto jana usiku.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (katikati),
akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu hatua
zilizofikiwa na serikali baada ya kutokea moto huo. Kulia ni Kaimu
Katibu Mkuu wa Wizara Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano, Gabriel Migile na kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi
wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Profesa Ninatubu Lema.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.
Paa la chumba kilichoungua.
Waandishi wa habari wakiangalia chumba hicho.
Chumba
namba mbili cha kutunzia mizigo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius
Nyerere (JNIA), kikiwa kimetekea kwa moto uliotokea jana usiku katika
uwanja huo.
Na Dotto Mwaibale
SERIKALI
imeunda tume ya watu 12 kwa ajili ya kuchunguza tukio la kuungua moto
chumba namba mbili cha kuhifadhia mizigo katika Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).
Akizungumza
katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa alisema tume hiyo
itaongozwa na Mwenyekiti wa Bodi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege
Tanzania (TAA), Joseph Nyahende.
"Tume
hiyo tumeipa muda wa mwezi mmoja ili kukamilisha uchunguzi huo ambapo
tutatoa taarifa kamili ya chanzo cha moto huo" alisema Mbarawa.
Akizungumzia
kuhusu tukio hilo alisema moto huo ulitokea jana usiku kwenye chumba
namba mbili cha kuhifadhia mizigo ya abiria katika uwanja huo hata hivyo
thamani ya vitu vilivyoungua bado haijajulikana.
Katika
hatua nyingine Waziri Mbarawa ameinyoonyea kidole kampuni inayofanya
kazi ya kupokea mizigo katika uwanja huo ya Swissport kuwa iache kufanya
njama za kuzuia kampuni ya Nas Dar Airco iliyopewa mkataba wa kazi
katika uwanja kufanya kazi vinginevyo serikali itaifutia leseni.
"Tunataarifa
kuwa nyinyi Swissport mnaizuia kampuni hiyo kufanya kazi nasema
badilikeni vinginevyo tutawafutia leseni yenu" aliagiza Profesa Mbarawa.
Profesa
Mbarawa alitoa maagizo kwa kampuni hiyo ianze kufanya kazi haraka
iwezekanavyo kama walivyokubaliana katika mkataba waliopewa.
Mkurugenzi
Mkuu wa Swissport Mrisho Yassin hakuweza kuzungumzia suala hilo kwa
wakati huo kutokana na mazingira yaliyokuwepo baada ya mkutano huo na
alipopigiwa simu baadaye muda wote simu yake ilikuwa ipo bize