RC MAKONDA AWATAKA WAKAZI WA DAR ES SALAAM KUJITOKEZA KESHO ENEO HILI,SOMA HAPO KUJUA
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam mh Paul Makonda
amewataka wana nchi wa Mkoa wa Dar es salaam, kujitokeza kwa wingi
kesho katika ufunguzi rasmi wa sehemu ya kwanza ya mradi wa mabasi ya
mwendo wa haraka /mwendo kasi DART , utakao fanywa kesho na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mhe.Dr John P Magufuli kesho January 25.
Amesema uzinduzi huo utakuwa ni mwendelezo wa
jitihada kubwa zinazo fanywa na serikali katika kutatua kero mbalimbali za
wananchi hasa katika kupunguza msongamano barabarani hapa mjini.
Mradi wa usafiri wa mabasi ya mwendo kazi ulianza
kutumika kwa kibali maalumu cha Rais Magufuli tangu tarehe10/5/2016 kwa
safari za kumara ,kivukoni ,morocco ambazo zinahusisha jumla ya kilomita
20.9 Ikiwa ni sehemu ya kwanza ya mradi huu
Ufunguzi huo utafanyika kuanzia saa 8:00 asubuhi
katika kituo cha DART Gerezani kariakoo