SSoko
la hisa la Dar es Salaam –DSE limesema kuwa ongezeko la hati fungani katika
soko hilo limetokana na baadhi ya wawekezaji kutafuta athari ndogo zaidi za bei
ya hisa.
Akizungumza na wanahabari Jijini Dar
Es Salaam Meneja biashara na mauzo Patrick Msusa amesema kuwa hatua hiyo ya
ongezeko la hati fungani limesababisha mauzo ya hisa katika soko hilo kushuka
kutoka shs 13.2 bilion mpaka kufikia shs 8bilioni.
“hatua hii pia imeweza kusababisha
makampuni matatu katika sekta ya mawasiliano kuingia katika orodha ya makampuni
ya simu yaliorodhoshwa katika soko letu la hisa, ikiwemo Vodacom, Tigo na
Airtel”. Alisema Patrick Msusa.
Vile vile ameongeza kwa kusema kuwa,
katika takwimu za soko hilo kwa kipindi caha wiki sita zilizopita ukubwa wa
mtaji wa makampuni ya ndani umeweza kupungua kwa asilimia 2.4% wakati kampuni
ya TBL ikiongoza kwa punguzo la asilimia 5% na sekta za kibiashara ikishuka kwa
asilimia 15.6% ambapo hatua hiyo imetokana na kushuka kwa hisa za benk ya CRDB.
Hata hivyo aliyataka makampuni ya
mawasiliano ya simu nchini kuweza kujiorodhesha kufuatia sheria ya serikali ya
kuyataka makampuni hayo kuuza hisa za zao kwa wananchi kupitia soko hilo ili
kukuza na kuchangia katika pato la taifa.
Ongezeko la hati Fungani limeathiri mauzo ya Hisa Nchini ,Mususa wa dse afunguka,soma hapo kujua
Reviewed by Unknown
on
19:41:00
Rating: 5