MUFTI ABUBAKARY ZUBERY ANAVYOPAMBANA KULETA UMOJA WA WAISLAMU
Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakary Zubery mapema hivi karibuni aliongoza mamia ya Waislamu wa madhehebu mbalimbali kushiriki katika Maulidi ya Mtume Muhammad(Rehma na amani ziwe juu yake) iliyoandaliwa na Taasisi ya Bilal Muslim Mission, sherehe iliyofanyika katika viwanja vya msikiti wa mdoe ulio karibu na mtaa wa Lumumba Jijini Daresalaam.
Sherehe hizo ambazo zilianza majira ya saa tatu usiku, ulishuhudia Masheikh wakubwa wa Ahlusunna , Masheikh wa wilaya zote za Dar es Salaam pamoja na walimu wa madrasa na wanafunzi wao.
Ujio wa Mufti Zubery kushiriki katika sherehe za Maulidi ya Mtume tena kwa dhehebu ambalo awali ilikuwa ni vigumu kuhudhuria inaelezwa ni ishara tosha kuwa Kiongozi huyo amedhamiria kuondoa ubagauzi uliopo kati ya kundi moja na lingine ambayo yote yanasema yanamfuata Mtume Muhammad.
Akizungumza na Fullhabari.com, Mmoja wa wadau waliohudhuria sherehe hizo amesema, kitendo anachofanya Mufti kinapaswa kupongezwa, akidai Waislamu wote Duniani wanaunganisha na Uislamu sambamba na karima ya La ilaha illallah Muhammadur Rasulullah.
Amesema, Waslamu wote ni ndugu wanapaswa kuwa wamoja hivyo jitihada zinazofanywa na Kiongozi huo ni nzuri kwa Umma wa Kiislamu.