HIVI NDIVYO RAIS WA GAMBIA ALIVYOONDOKA NCHINI MWAKE,SOMA HAPO KUJUA

Aliyekuwa Rais wa Gambia, Yahya Jammeh ameondoka
nchini humo baada ya mvutano wa muda kufuatia kushindwa katika uchaguzi mkuu wa
nchi hiyo uliofanyika Disemba Mosi mwaka jana.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na ECOWAS,
kiongozi huyo aliyeiongoza Gambia kwa miaka 22 alipanda ndege kuelekea nchini
Guinea ambapo akifika atasafiri kwenda nchini Equatorial Guinea atakapoishi
uhamishoni.
Yahya Jammeh is to go into exile in Equatorial
Guinea
Jammeh alishindwa na kiongozi wa upinzani, Adama
Barrow ambaye amekuwa akiishi nchini Senegal na kueleza kuwa atarudi Gambia
usalama ukiimarika.
Barrow aliyeapishwa katika Ubalozi wa Gambia nchini
Senegal, alisema kuwa akiingia madarakani ataunda tume kuchunguza ukiukwaji wa
haki za binadamu uliofanywa na Yahya Jammeh katika kipindi cha miaka 22 ya
utawala wake.
Rais wa ECOWAS, Marcel de Souza pia ameeleza kuwa
wanajeshi waliokuwa wametumwa kutoka nchi wanachama kwenda kumuondoa Jammeh
madarakani sasa wataondolewa japo wachache watabaki kuendelea kuimarisha usalama.
Wananchi wa Gambia wamekuwa na hisia tofauti kuhusu
kuondoka kwa Jammeh ambapo wanaoaminika kuwa ni wafuasi wake walisikitika kwa
majonzi alipokuwa akiwaaga katika uwanja wa ndege huku wengine wakishangilia
kuamini kuwa ni mwisho wa utawala wa kidikteta uliokuwa hauheshimu haki za
binadamu.
Kitu alichoahidiwa Jammeh kuweza kuachia madaraka
baada ya kukutana na baadhi ya viongozi wa mataifa mengine bado hakijafahamika.
Yahya Jammeh anakuwa Rais wa kwanza wa Gambia
kuondoka madarakani kwa amani tangu walipopata uhuru mwaka 1965.
a