CUF YA LIPUMBA YAENDELEZA HUJUMA KWA UKAWA,CHADEMA YAWATOA HUFU WAPIGA KURA,SOMA HAPO
ATHARI ya mtifuano ndani ya Chama cha Wananchi (CUF)
zinaendelea ambapo sasa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kinawinda
kura za CUF, anaandika Christina Haule.
Chadema
mkoani Morogoro kimeomba wanachama wa CUF wanaounga mkono chama hicho kwenye
uchaguzi mdogo wa udiwani katika Kata ya Kiwanja cha Ndege kukipa kura Chadema.
Hatua hiyo inakuja baada ya Chadema kudai kwamba,
mgombea wa CUF kwenye kata hiyo Mlapokolo anahujumu Umoja wa Katiba ya Wananchi
(Ukawa) kwa kuungana na Prof. Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa CUF anayetambuliwa
na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini.
Prof. Lipumba amekuwa akizunguka kwenye kata
mbalimbali za uchaguzi Tanzania Bara kuwanadi wagombea wa udiwani kwenye
uchaguzi mdogo unaotarajia kufanyika kesho.
Kiongozi huyo wa CUF amekuwa akizunguka na wale
wanaomuunga mkondo ndani ya chama hicho kilichopasuka vipende viwili kutokana
na mgogoro wa kiuongozi unaotawala kwa sasa.
Miongoni mwa viongozi wanaomuunga mkono Prof.
Lipumba ni pamoja na Magdalena Sakaya, Naibu Katibu Mkuu CUF anayetambuliwa na
Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa na Abdul Kambaya, Naibu Mkurugrnzi wa
Mawasiliano na Umma wa chama hicho.
Chadema katika Kata ya Kiwanja cha Ndege, Morogoro
kikimnadi mgombea wake Salum Milindi kimedai kuwa, Mlapakolo anauza utu wake
kwa kumuunga mkono Prof. Lipumba na Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Kauli hiyo imetolewa na Matwew Mlipina, Kiongozi wa
Chadema Makao Makuu ya chama hicho Morogoro jana na kwamba, Mlapakola ni
mamluki.
Mlipina amedai kwamba, Prof. Lipumba ni mamluki wa
CCM tangu mwaka 1992 baada ya kusababisha kuvunjika kwa kamati kwenye kikao cha
kujadili katiba wakati akigombania fedha.
Na kwamba, ili Mlapakolo alinde heshima yake
anapaswa kujitoa huko kwanza kwa kuwa, wakati huu haeleweki kwa wananchi.
Hivyo aliwaomba wanachama wa CUF kuwa na uamuzi
sahihi na kumchagua Milindi ili aweze kuwaongoza sababu ana nguvu, nia na uwezo
wa kuwasaidia na kuleta maendeleo kwa wanakiwanja cha ndege.
Elisa Ninja, Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Kati
|(Morogoro, Dodoma na Singida) amewasihi wakazi wa kata hiyo kumchagua
mgombea wao katika uchaguzi huo ili kuweza kupata maendeleo ya kweli.
Hata hivyo, ameliomba Jeshi la Polisi nchini, kuona
umuhimu wa kufanya kazi yao bila upendeleo kwa kutatua sawa matatizo na
migogoro ya kisiasa yanayojitokeza kuanzia ngazi ya kata hadi Taifa.
Mgombea wa udiwani kata hiyo Milindi amewaomba wananchi
wa kata hiyo kumchagua na kuwa kiongozi wao huku akiahidi kutatua kero
mbalimbali zilizopo kwenye kata hiyo na kuwaletea maendeleo.