Diamond akabidhiwa bendera ya taifa kuliwakilisha taifa AFCON 2017 nchini Gabon
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Moses Nnauye
(kushoto) akimkabidhi bendera ya Taifa Mwanamuziki wa bongo fleva Nasib
Abdul maarufu kama Diamond Platinumz kwa ajili ya kwenda kuiwakilisha
Tanzania kwenye Ufunguzi wa Mashindano ya AFCON 2017 yanayotarajiwa
kufanyika nchini Gabon.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Moses Nnauye akiongea
na wageni waalikwa pamoja na Waandishi wa Habari wakati wa hafla ya
kumkabidhi bendera ya Taifa mwanamuziki wa Bongo Fleva Nasib Abdul
maarufu kama Diamond Platinumz anayekwenda kushiriki katika Ufunguzi wa
Mashindano ya AFCON 2017 yanayotarajiwa kufanyika nchini Gabon. Hafla
hiyo imefanyika leo 11 Januari, 2017 Hoteli ya Serena Jijini Dar es
Salaam.
Wageni
waalikwa pamoja na Waandishi wa Habari wakifuatilia hotuba ya Waziri
Nape Nnauye wakati wa hafla ya kukabidhi bendera ya Taifa kwa
mwanamuziki wa Bongo Fleva Nasib Abdul maarufu kama Diamond Platinumz
iliyofanyika leo 11 Januari, 2017 Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
wa DSTV Multi Choice Tanzania Bw. Salum Salum akiongea na Waandishi wa
Habari pamoja na wageni waalikwa wakati wa hafla ya kukabidhi bendera ya
Taifa kwa mwanamuziki wa Bongo Fleva Nasib Abdul maarufu kama Diamond
Platinumz anayekwenda kushiriki katika Ufunguzi wa Mashindano ya AFCON
2017 yanayotarajiwa kufanyika nchini Gabon.
Balozi
wa DSTV Bomba Bw. Lucas Mhuvile maarufu kama Joti akiongea na Waandishi
wa Habari pamoja na wageni waalikwa wakati wa hafla ya kukabidhi
bendera ya Taifa kwa mwanamuziki wa Bongo Fleva Nasib Abdul maarufu kama
Diamond Platinumz iliyofanyika leo 11 Januari, 2017 Hoteli ya Serena
Jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Moses Nnauye,
Mkurugenzi wa DSTV Multi Choice Tanzania Bw. Salum Salum pamoja na
mwanamuziki wa bongo fleva Nasib Abdul maarufu kama Diamond Platinumz
wakiteta jambo kabla ya kuanza kwa hafla ya kukabidhi bendera ya Taifa
kwa mwanamuziki huyo anayekwenda kushiriki katika Ufunguzi wa Mashindano
ya AFCON 2017 yanayotarajiwa kufanyika nchini Gabon.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Moses Nnauye
(katikati) akimpongeza mwanamuziki wa bongo fleva Nasib Abdul maarufu
kama Diamond Platinumz wakiteta jambo kabla ya kuanza kwa hafla ya
kukabidhi bendera ya Taifa kwa mwanamuziki huyo anayekwenda kushiriki
katika Ufunguzi wa Mashindano ya AFCON 2017 yanayotarajiwa kufanyika
nchini Gabon. Anayeshuhudia kushoto ni Mkurugenzi wa DSTV Multi Choice
Tanzania Bw. Salum Salum
Mwanamuziki
wa bongo fleva Nasib Abdul maarufu kama Diamond Platinumz akimshukuru
Waziri Nape Nnauye pamoja na Serikali kwa ujumla kwa mchango mkubwa
inaotoa katika kukuza sekta ya Sanaa nchini wakati wa hafla ya kukabidhi
bendera ya Taifa kwa mwanamuziki huyo anayekwenda kuiwakilisha Tanzania
kwenye Ufunguzi wa Mashindano ya AFCON 2017 yanayotarajiwa kufanyika
nchini Gabon.iliyofanyika leo 11 Januari, 2017 Hoteli ya Serena Jijini
Dar es Salaam.