WAZIRI UMMY MWALIMU NA WIZARA YAKE YAJITOSA KUMALIZA TATIZO LA MAGONJWA YSIYO YA KUAMBUKIZWA,SOMA HAPO KUJUA
![]() |
Pichani ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu Picha na Maktaba |
Katika kuhakikisha Watanzania wanakuwa na utaratibu
wa kujihusisha na mazoezi ili kupunguza hatari ya kupata magonjwa ambayo sio ya
kuambuza, Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto imesema kuwa kampeni ya kuhamasisha mazoezi ya AFYA YAKO, MTAJI WAKO,
FANYA MAZOEZI, LINDA AFYA YAKO itakuwa endelevu na itafanyika nchi nzima.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakati akifunga mafunzo ya siku
moja kwa waandishi wa habari yaliyokuwa yanalenga kutoa elimu kwa wanahabari
kuhusu magonjwa yasiyo ya kuambukiza.
“Kila mwezi tutakuwa tukichagua mkoa ambao mazoezi yatakuwa
yanafanyika na yatakuwa yakiongozwa na mimi, au naibu waziri au katibu mkuu
naibu katibu mkuu au hata viongozi wengine na hakutakuwa na gharama maana
tunajua tukianza kuweka hayo mambo kutajitokeza changamoto nyingine,”
alisema Ummy.
Waziri Ummy alisema alifikia uamuzi wa kuanzisha
kampeni hiyo kutokana na takwimu kuonyesha kuwepo kwa idadi kubwa ya watu ambao
wamekuwa wakipoteza maisha kutokana na magonjwa yasiyo ya kuambikiza na wakati
ni jambo ambalo linaweza kumalizika kama wananchi watabadili mfumo wao wa
maisha na kuanza kuwa wanafanya mazoezi.
Nina mwaka hapa wizarani wakati nimefika kipaumbele changu
kilikuwa ni afya ya mama na mtoto lakini kumbe tukasahau upande mwingine,
ripoti inaonyesha kati ya watu 100 ambao wanapoteza maisha, 27 wanakufa
kutokana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza, sasa niamua lazima tulishughulikie
jambo hili,” alisema Waziri Ummy.
Pia aliwataka Watanzania wote kujitokeza Desemba, 17
katika viwanja vya Leaders Club kuanzia saa 12:30 asubuhi katika uzinduzi wa
kampeni ya kitaifa ya kudhibiti magonjwa yasiyo ya kuambukiza ambapo mgeni
rasmi atakuwa Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan