HUMPHREY AKABIDHIWA MIKOBA YA CCM RASMI,SOMA HAPO KUJUA

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi
(CCM) Humphrey Polepole amesema atahakikisha chama hicho kinakuwa ni cha
wanyonge na kuendelea kuwa kimbilio la wasio na sauti.
Polepole ametoa kauli hiyo leo wakati akikabidhiwa
rasmi ofisi na Katibu anayemaliza muda wake Nape Nnauye katika ofisi
ndogo za Makao Makuu ya chama hicho Lumumba jijini Dar es Salaam.
Polepole alisema kwa misingi ya chama hicho
imejengwa kuwasaidia na kuwa tete wanyongo hivyo katika muda wake wa uongozi
atahakikisha chama kinasimama katima misingi hiyo ya kuanzishwa kwake.
“Msingi wa chama chetu ni utetezi wa wanyonge,
tutahakikisha kinaendelea kuwa kimbilio la wasio na sauti,” alisema Polepole.
Aidha, katibu huyo alisema kuwa katika kutekeleza
majukumu yake aliyokabidhiwa leo na mtangulizi wake, atahakikisha anajikita
zaidi katika kazi za itikadi zaidi kuliko uenezi kwa kuwa itikadi ndiyo
inayokibeba chama.
Polepole alitumia muda huo kumshukuru Nape Nnauye
anayemaliza muda wake na kusema kuwa ni kiongozi imara na kuwa katika muda wake
aliweza kuitumikia vyema nafasi yake. Lakini pia alisema japo anamaliza muda
wake, lakini atakuwa akimuhitaji mara kwa mara kwa ajili ya ushauri na mambo
mengine.
Wakati huo huo, Polepole amemshukuru Mwenyekiti wa
CCM Dkt John Pombe Magufuli na Halmashauri Kuu ku kumwamini na kumpa majukumu
hayo makuwa.