MAMBO YAANZA KUMWENDEA HOVYO ZITTO KABWE,VIGOGO WAANZA KUMSUSIA CHAMA,SIRI YA YOTE YAFICHUKA,SOMA HAPO KUJUA
![]() |
Pichani Aliyekuwa mratibu wa Kampeni wa ACT-Wazalendo,Nixon Tugara akiwa ameshikilia kadi ya Chama cha Mapinduzi CCM baada ya kutangaza rasmi kuhamia chama hicho, |
NA KAROLI VINSENT
CHAMA cha ACT-Wazalendo ni wazi kinapitia katika
hali mbaya ndivyo naweza kusema baada ya Vigogo wa juu wa Chama hicho,kuanza
kukiacha chama hicho na kuhamia Chama cha mpinduzi (CCM) huku baadhi yao
kutangaza kuachana na siasa.(Fullhabari.blog unaripoti)
Hayo yamebainika leo Baada Vigogo wengine kukihama chama hicho ambacho kinaongozwa na Zitto kabwe ambapo Aliyekuwa mratibu wa Kampeni wa
ACT-Wazalendo,Nixon Tugara kutangaza Rasmi kujiunga na CCM kwa madai ya kuchoshwa
na Chama chake cha hicho kwa kutokuwa na sera za kueleweka.
Tugara amejiunga CCM na kupokera na katibu Mkuu wa
chama hicho,Abdalraman Kinana wakati katibu huyo alipokuwa akizindua jengo la
CCM liliopo Upanga Jijini Dar es Salaam,
Mbali na Tugara mwanachama mwengine ni mwenye
ushawishi ambaye amekihama chama Chama ACT-Wazalendo ni msanii Afande Selle
ambaye pia aligombania ubunge kupitia Chama hicho kupitia jimbo la Morogoro
Mjini,
Selle ambaye yeye ni tofauti na Tugara,amesema
anaachana na chama chake na kuachana na siasa ,
Msanii huyo ametangaza hatua hiyo kupitia ukrasa
wake wa Faceebook amesema anaachana na chama chake na kuwa mtu wa kawaida
ambaye hatajihusisha na siasa huku akisema uamuzi wake usichukuliwe vibaya,
Kuhama kwa wanachama hao kuna kuja ikiwa ni mwezi
mmoja kupita kushuhudia Vigogo kadhaa wakikacha chama hicho,vigogo hao ni aliyekuwa Mgombea Ubunge kupitia Chama hicho kwenye
jimbo la Kasulu Mjini,David Machali kutangaza kukihama chama hicho na kuhamia
CCM kwa madai ya kukoshwa na sera za rais John Magufuli katika kupambana na
ufisadi.
Mbali na Machali yupi Kigogo wa juu wa chama hicho
aliyetangaza kuachana na chama hicho ni Aliyekuwa Katibu wa Bunge na Serikali za Mitaa katika Sekretarieti ya Chama cha ACT-Wazalendo,Habibu Mchange ambaye ametangaza rasmi
kuachana na Chama hicho na kujikita katia kazi za ujasiliamali.
Kwa mujibu wa Kigogo wa juu aliyendani ya Chama
hicho ambaye hakutaka jina lake litajwe mtandaoni aliumbia mtandao wa
(Fullhabari.blogs) sababu ya Viongozi kukihama chama hicho kumetokana na chama chake hicho kutokuwa na mwelekeo huku akitoa
tahadhari kuwa kama viongozi wenzake wasipobadilika basi tutashudia vigogo
wengi watakihama chama chama hicho.
Amedai chama hicho kutoleweka wapi wapo na nini
wanachokitaka kwani jambo hilo linakihalibu Chama.
“Ninachokwambi sahivi Chama hakina ajenda,leo chama
hakieleweki hiki ni Chama cha Upinzani au chama gani,maana unakuta Chama badala
ya kuungana na vyama vya upinzani kupambana na kukiondoa chama cha CCM lakini
badala yake unakuta chama kimekuwa kinafurahi migogoro ya vyama vya
upinzani,wakati huo huo wanakiponda chama cha CCM”
Ameongeza kusema “Wewe unategemea nini mwaka jana
kwenye uchaguzi sababu hii imepeleka chama kufanya vibaya mno,leo hata malengo
ya kupata wabunge wengi ili tuwe na ruzuku tumekosa,sahivi chama kinahali mbaya
kifedha hata kulipa watendaji mishahara tumeshindwa,wewe unategemea nani
atabaki watahama wengi kama wasipobadilika viongozi wa juu’”kimesema Chanzo
chetu hicho.