NAPE AWAOMBA MSAMAHA VYAMA VYA UPINZANI,SOMA HAPO KUJUA

Alikuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha
Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye amewaomba radhi viongozi na wafuasi wa vyama vya
upinzani nchini kwa lolote ambalo aliwakwaza wakati akitekeleza majukumu yake
katika nafasi hiyo.
Nape amewaangukia wapinzani pamoja na makundi
mengine ya watanzania ikiwemo viongozi wenzake ndani ya chama leo wakati
akikabidhi rasmi ofisi kwa kiongozi mpya anayechukua nafasi hiyo, ambaye ni
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Dar es Salaam, Humphrey Polepole katika ofisi ndogo za
makao makuu ya chama hicho, Lumumba Jijini Dar es Salaam.
"Nawaomba msamaha viongozi wenzangu, wanachama,
waandishi na hata wapinzani pale ambapo nimewaumiza katika kufanya kazi yangu,
samahani sana. Nategemea ushirikiano niliopatiwa mimi na wanahabari utaendelea
kwa ndugu yangu Humphrey Polepole, ni mtu mwenye weledi mpana" amesema
Nape
Nape pia amekiri kuwa chama hicho kimemsaidia zaidi
kwenye maisha yake kuliko yeye alivyokisaidia wakati akiitumikia nafasi hiyo.
"Nakiri mbele yenu kuwa chama kimenisaidia
zaidi kuliko mimi nilivyokisaidia Chama, nashukuru Mungu kuwa nimemaliza kazi
hii salama, nilipata wosia wa Mzee Kinana kuwa nishukuru nikimaliza
salama"