WANAWAKE NCHINI WANAONGOZA KUWA NA UGONJWA WA UKIMWI,SOMA RIPOTI YOTE HAPO,KWA KUBOFYA HAPO
NA KAROLI VINSENT
WAKATI ,Dunia leo Tarehe 1 Desemba, ikiazimisha siku
ya ukimwi Duniani,inaelezwa kuwa Hali ya Maumbukizo ya ukimwi hapa nchini kwa upande wa Bara inaonyesha kuwa wanawake ndio
kinara wa kwa maambukizo wa ugonjw
a wa ukimwi kuriko wanaume.
Ambapo Tafiti inayonyesha asilimia 6.2 ya waathirika
ni wanawake huku wanaume wakiwa ni
asilimia 3.8 .
Huku pia tafiti hiyo ikionyesha jumla ya watu
1,538,382 wamebainika kuishi na VVU hapa nchini,huku ikitajwa Vijana wenye umri wa kati ya miaka 15
hadi 24 ni asilimia 10.6 na watoto waliochini ya miaka 15 ni 11.8 ya watu
wanaoishi na VVuU nchini.
Hata hivyo,Tafiti zinaonyesha kuwa kati ya idadi
hiyo wanaoishi na virusi vya ukimwi asilimia 50 ndio wanapata dawa za kupunguza
makali ya VVU .
Akisoma Taarifa hiyo wakati wa mkutano na waandishi
wa habari leo Jijini Dar es Salaam,Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri mkuu
(Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na watu
wenye Ulemavu)Jestina Mhagama amesema licha ya ukimwa kutajwa bado ni janga
hapa nchini na Duniani kutoke tafiti zinaonyesha maambukizo mpaya ya ukimwi
yanadiriwa kufikia 48,000 kwa mwaka.
“Ukimwi bado ni Janga kubwa duniani na hapa
nchini,Dunia imejiwekea lengo la kutokomeza Ukimwa kama janga ifikapo 2030,ili
kufikia lengo hilo,yapo mashirika duniani yamejiwekea yakushirikiana na nchi
mbali mbali kutokomeza ugonjwa huo”amesema Waziri Mhagama.
Waziri Mhagama amesema kwa sasa serikali nchi
imeendelea kufanya jitihada mbali mbali za kuhakikisha jamii inaondokana na
ugonjwa huo kwa kuwahimiza wananchi kuendelea kupima afya zao ili wajitambue na
kujua namna ya kujilinda.
“Licha ya kuwahimiza watu wajitokeza kupima afya
zao,pia serikali inatoa wito kwa wale ambao watakutwa na maambukizo ya
VVU,waanzishiwe huduma ya dawa za
kufubaza virusi vya UKIMWI, mara moja ili waweze kuishi maisha marefu na
yaliyojaa na afya bora’ameongeza kusema Waziri Mhagama.
Hata hivyo,Waziri Mhagama amesema kwa sasa serikali
imeanzisha mfuko wa ukimwi ambapo umepitishwa na bunge kwa sheria namba 6 ya
mwaka 20015 kwa lengo la kuhakikisha uwepo wa rasimali za kutosha katika
kupambana na ugonjwa huo hapa nchini.
Kwa upande wake Dr,Angella Ramandani ambaye ni
Meneja mipango wa (National Aids Contoll Program)amesema kwa sasa serikali
imefanya jitihada mbali mbali za kuhakikisha dawa za kufubaza za birusi vya
ukimwi zinapatikana kwa wakati ili wanaondulika na ugonjwa huo iwasaidie.
“Napenda niwatoe hofu wanaogundulika na ugonjwa wa ukimwa,jamani dawa zipo
mahospitali,nawakikishia wananchi dawa
zipo,na bule kabisa”amefafanua Dr Angella.