JINSI SHIA ITHNASHERIYA TANZANIA WALIVYOADHIMISHA KIFO CHA MTUME MUHAMMAD (S.A.W.W) MWEZI 28, SAFAR 1438.
Kiongozi Mkuu wa Waislam Dhehebu la Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala akiongea na Waandishi wa Habari katika Matembezi ya Amani ya Kuadhimisha Kumbukumbu ya Kifo cha Mtume Muhammad (s.a.w.w) Kigogo Round About, Leo Jijini Dar es salaam.Ambayo yalianzia Ilala Boma hadi Uwanja wa Pipo Kigogo. |
Dhehebu la Shia Ithnasheria Tanzania wameungana na Waislamu wengine Duniani kuazimisha Kifo cha Mtukufu wa Daraja, Kipenzi cha Waislamu Mtume Muhammad (S.A.W.W),kwa njia ya maandamano kutoka eneo la Ilala Boma Hadi viwanja vya Pipo vilivyopo Kigogo Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari, Round about ya Kigogo Kiongozi Mkuu wa Dhehebu hilo, Sheikh Hemed Jalala amesema mnamo mwezi 28, Mfungo tano Hijjiria Kiongozi wa watu wote Duniani Mtume Muhammad ndipo alipoaga Dunia.
Aidha akitaja sababu za kufanya kumbukizi hizo, Sheikh Jalala amesema kuna sababu Nyingi za kukumbuka matendo ya Mtume Nyakati za uhai wake, kwani yeye ndiye huruma kwa umma wote.
Maandamano hayo
yamefanyika Jijini Dar es Salaam na kuongozwa na Kiongozi Mkuu wa kiroho wa waislam wa dhehebu la Shia ITHNASHERIYA Tanzania Sheikh HEMED JALALA na kuhudhuriwa na mamia ya waumini wa
dhehebu hilo.
" Tuna sababu nyingi za kumkumbuka Mtume Muhammad, lakini niseme sababu mbili
tatu kwa harakaharaka, Sababu ya kwanza kama anavyosema Mwenyezimungu katika
Qur’an kwamba “Wewe tumekutuma ukawe ni huruma kwa watu wote” sio huruma kwa
Waislam. Sasa unapomuangalia Mtume Muhammad (s.a.w.w)
wakati bado yupo hai, akiwa yuko katika mji wa makka na baada ya kuwa madina,
tulimpata mtume alikuwa na huruma kwa watu wote, mtume alikuwa huruma kwa
wasiokuwa waislam, mtume alikuwa na huruma kwa waislam, mtume alikuwa huruma
kwa wtu waliokuwa wanaabudu masanamu, kwa watu waliokuwa wanaabudu lata,
wanaabudu manata na wanaabudu hubal," Alisema Sheikh Jalala
Maandamano yakiendelea.