UCHAGUZI WA ZANZIBAR WAINGIA GIZANI,SOMAHAPO KUJUA
WAKATI kampeni za uchaguzi mdogo wa Jimbo la Dimani,
Zanzibar zikiwa zimeanza, Juma Ali Juma mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),
amemkatia rufaa kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Abdulrazak Khatib Ramadhan
mgombea wa Chama cha Wananchi CUF. Anaandika Pendo Omary …
(endelea).
Hatua
hiyo inatajwa kama mwendelezo wa mbinu za kuhakikisha mgombea wa CCM anapita
bila kupigwa na mpinzani wake mkuu katika uchaguzi huo ambaye anatoka CUF.
Juma amekata rufaa hiyo akipinga uamuzi wa msimamizi
wa uchaguzi wa Wilaya ya Magharibi ambaye alilitupa pingamizi lake hapo awali
dhidi ya Ramadhan.
Katika pingamizi hilo, mgombea wa CCM anadai kwamba
mpinzani wake kutoka CUF hakupitishwa na vikao halali vya chama cha CUF hivyo
hafai kushiriki katika uchaguzi huo.
Hata hivyo, Fatma Gharib Haji msimamizi wa uchaguzi
huo, amenukuliwa akisema, “mgombea wa CCM aliwasilisha pingamizi dhidi ya
mgombea wa CUF ambayo yalitupwa, baada ya kuonekana hayakuwa na mashiko.
Hatimaye wagombea wote wakapewa fomu za kuwapitisha.”
Fatma amesema utaratibu kuhusu rufaa hiyo unaihusu
Ofisi ya Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi ambayo ndiyo itakayosikiliza katika
muda utakaopangwa.
Awali mgombea wa CUF aliweka pingamizi kuwa mgombea
wa CCM akidai kuwa katika kiapo chake hakutaja mali zake. Pingamizi hilo pia
lilitupwa na NEC kwa madai kuwa halina mashiko.