SUALA LA USHOGA LAITESA WILAYA YA TEMEKE,WATOTO WADOGO WATAJWA KUJIINGIZA KWENYE MAMBO HAYO,SOMA HAPO KUJUA
WAKATI serikali nchini ikitangaza kuzifuta taasisi
zote ambazo zinatetea masuala ya ushoga ndani ya nchi,Imeeleza hali ipo tofauti
baada ya kuripotiwa kuwepo vitendo vya ushoga
huku ikitajwa watoto Vijana chini ya miaka 20 ndio waathirika zaidi na vitendo
hivyo ambapo inatajwa wazazi wa vijana hao wamekuwa wakichangiwa kuwepo kwa
hali hiyo.
Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na
Mwenyekiti wa mtaa wa Keko Machungwa wilaya ya Temeke jijini hapa,Mashaka
Hamadi wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye kampeni yakutoa elimu
kwa watoto wadogo ambapo Kampeni hiyo iliandaliwa na wanafunzi wa Chuo kiku
kishiriki cha Mlimani (DUCE)
Ambapo Hamadi amewaaeleza wanahabari kuwa katika
kata yake hiyo kuomeongezeka kwa kasi vitendo vya ushoga .
“Yaani katika katika kata yangu vitendo vya ushoga
vimeongezeka kwa wingi sana hususani watoto wadogo ,wamekuwa wakifanya vitendo
hivyo”amesema Hamadi
Amesema sababu kubwa iliyochangiwa kuongezeka kwa
vitendo hivyo kumechangiwa na wazazi wa watoto hao kuwaingiliwa kinyume na
maumbile watoto hao jambo analodai limechangiwa kuongezeka kwa vitendo hivyo.
Ametolea mfano katika kesi tano ziripotiwa za
ubakaji katika kata yake hiyo
amedai kesi tatu ni za kulawitiwa
kwa watoto wa kiume.
Kwa upande wake Diwani wa Kata hiyo Muburani ,Juma Mkenda amesema hali ya vitendo
vya ushoga ipo katika maeneo yake huku akiitaka serikali kuingilia kati kwa
kuwachukulia hatua watu wanahusika na vitendo hivyo.