Zinazobamba

RAIS WA MAREKANI AIPIGA VIJEMBE SHIRIKA LA UMOJA WA MATAIFA,SOMA HAPO KUJUA

DONALD Trump Rais mteule wa Marekani amesema Shirika la Umoja wa Mataifa (UN), limeshuka hadhi kwa kiasi kikubwa na nguvu yake inazidi kupungua kadri muda unavyoenda. Anaandika Wolfram Mwalongo … (endelea).
Trump ameeleza hayo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Twitter akidai vikao vya UN hukutanisha watu kwa madhumuni ya kupiga soga badala ya kushughulikia mambo mubimu.
Hatua ya kiongozi huyo kuikebehi UN imekuja ikiwa ni siku chache tangu Baraza la Usalama la UN kuionya Israel kuacha kujenga makazi ndani ya mpaka wa Palestina, huku Trump akiunga mkono kitendo hicho.
“Sifikiri kama Israel inapaswa kusimama,” alisema Trump kuhusu suala hilo.
Baraza la hilo limesema Israel inakiuka sheria za kimataifa kwa kujenga ndani ya ardhi ya Wapalestina.
Tayari Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa Israel amethibitisha kufanyika kwa ujenzi wa nyumba zaidi ya 200 ndani ya Palestina jambo ambalo linahofiwa kuwa huenda likachochea uhasama baina ya mataifa hayo hasimu.